Shutdown Academy

60 dakika

Kichwa cha Kosi : Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao

WITNESS
Muhtasari:
Kosi hii inatoa muongozo wa jinsi ya kunakili ukiukaji wa haki za binadamu kwa njia salama na vizuri zaidi kwa kutumia vidio wakati wa kuzimwa mtandao. Inayowalenga wanaharakati wa mashinani, kosi hii inatoa ushauri wa vitendo ambao watu ama mashirika madogo yaliyo na raslimali finyu wanaweza kutunga.
Kuhusu kozi hii:
Serikali za kidhalimu, kwa kushiriana na kampuni za mawasiliano, kwa kiasi kikubwa wanageukia kuzima mtandao kama njia ya kukandamiza watu wake, kuzuia uhamasishaji na kuzuia kunakiliwa na kusambazwa kwa taarifa kuhusu ukiukaji wa haki za binadmu. Kati ya Januari na Mei mwaka wa 2021 pekee, muungano wa #KeepItOn ulirekodi visa 50 vya kuzimwa mtandao kote ulimwenguni, vikiwemo visa vya kuzimwa huko wakati wa shughuli muhimu kama uchaguzi wa Uganda, mapenduzi ya Myanmara na kulipuliwa Israeli katika ukanda wa Gaza.
Najifunza nini:
Kosi hii inanuia kuwapa watu na makundi vidokezo vya vitendo vya kuendelea kunakili ukiukaji wa haki za binadamu kutumia vidio licha ya kuzimwa mtandao. Katika kila sura, kosi hii inaeleza mbinu na zana zinazoweza kusaidia wanaonakili kuwa salama zaidi na kuhakikisha kuwa nakala zao zinahifahiwa, zinaweza kuthibitishwa na kuwafikia wengine hata bila kuweza kutumia intaneti
Ni nini nafaa kujua:
Kosi hii hahitaji ujuzi wowote maalum, lakini inaangazia haswa kuhusu vipengele vya unakili wa vidio ambao unaathiriwa na kuzimwa mtandao badala ya unakili wa vidio kwa ujumla.

Walimu

Yvonne Ng

Yvonne Ng is an audiovisual archivist and the Archives Program Manager at WITNESS. Working at the intersection of human rights, technology, and human rights, Yvonne supports and trains grassroots activists on collecting, managing, and preserving video evidence for advocacy and evidence. Yvonne holds an MA in Moving Image Archiving and Preservation from New York University.

1.1 Utangulizi katika kosi
1.2 Mbona unakilizaji vidio / vidio kutumiwa kuwa ushahidi
1.3 Swali: Kunakili vidio kama ushahidi
2.1 Tayarisha Simu Yako kwa Uwekaji Nakala bila Mtandao - utangulizi
2.2 Usalama wa simu
2.3 Vidokezo vya ziada vya kiusalama na vidokezo vya kuficha viunzi/uandaaji nyaraka zako
2.4 Kuchagua viunzi vya uandaaji nyaraka-Maswali ya kujiuliza
2.5 Installing / sharing apps without internet
2.6 Kikumbusho: jitayarishe huku ukiwa una mtandao
2.7 Mfano Ulioko: Ni Vipi Wanharakati wa Uganda wanajiandaa kwa kuzimwa Mtandao?
3.1 utangulizi – changamoto za kudumisha vidio zenye ushahidi wakati wa mtandao umezimwa
3.2 jinsi ya kufanya vidio yako iwe ya kuthibitika
3.3 kuweka akiba vitu vyako bila mtandao au tarakilishi
3.4 Mfano ulioko: Uhifadhi wa Ushahidi wakati wa kuzimwa Mtandao kule Latin America
3.5 Vidio kama ushahidi wa unyanyasaji wakati wa uchaguzi mkuu nchini Uganda
3.6 Maintaining verifiable video during a shutdown
4.1 Kushea na Bluetooth, Wifi Direct, na Nearby Share
4.2 Kushiriki kwa Kutumia Hifadhi Isiyochomekwa au Mtandao Usiochomekwa
4.3 Kutumia zana za P2P kwa mawasiliano na usambazaji
4.4 Kukwepa tovuti zilizozuiwa: sava za VPNs na DNS
4.5 Kukwepa kuzima kwa mtandao nchini Cuba na nchi nyingine huko Kusini Marekani.
4.6 Kukabiliana na Vurugu za Nchi na Kauli za Uongo za Serikali kuhusu Kuzimwa Mtandao nc
5.1 Vidio ya kumalizia
5.2 Uchunguzi wa kozi

Kozi zinazohusiana

  • 90 dakika

    Shutdown Academy

    Kupima Udhibiti wa Mtandao ukitumia zana za OONI na data huru

    Open Observatory of Network Interference (OONI)

    90 dakika

    Open Observatory of Network Interference (OONI)
  • 60 dakika

    Shutdown Academy

    Utangulizi kuhusu uzimaji mtandao

    Access Now

    60 dakika

    Shutdown Academy

    Utangulizi kuhusu uzimaji mtandao

    Access Now

usomaji unaopendekezwa

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
  • Faragha
  • Maagizo