Macho kwenye kuzimwa kwa mtandao

Yaliyomo: 

Utangulizi wa jinsi ya Kuweka Nyaraka Wakati Mtandao Umezimwa
Kutayarisha Simu kwa Uwekaji Nyaraka Bila Mtandao
Naweza Kutumia hiki Kiunzi (App) cha Nyakara?
Kudumisha Vyombo vya Habari Halali Wakati wa Kufungwa kwa Mtandao
Kuimarisha Habari Za Simu Bila Mtandao au Tarakilishi 
Upeanaji wa Faili na Mawasiliano Wakati wa Kuzimwa kwa Mtandao.

 

Mwezi Juni 2019, ambapo kuliendelea ukiukaji wa haki za binaadamu na majanga ya kibinaadamu nchini Myanmar, Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano nchini humo iliagiza kampuni za mawasiliano kuzima huduma za mtandao wa simu katika baadhi ya maeneo ya Jimbo La  Rakhine na Jimbo la Chin. Wakiashiria “kuvurugika kwa amani” na “shughuli haramu,” serikali ya Myanmar inadai kuwa ilitunga sheria hiyo ya kuzima  “kwa manufaa ya watu.” Kihalisia,kuzimwa huko kulizuia zaidi ya watu milioni moja kupata taarifa muhimu na mawasiliano, na kuvuruga shughuli za kibinaadamu. Jinsi Matthew Smith kutokaFortify Rightsalidai, “Kuzimwa huku kunatokeakwa mauaji ya halaiki yanayoendelea dhidi ya Rohingya na uhalifu wa kivita dhidi ya Rakhine, na hata kama ililenga wapiganaji, ni ya kutamausha.”

Kuzimwa huko kuliondolewabaadhikatikamiji mitanomnamo Septemba 2019, japokuwa kunaendelea.  Katika mwezi huo huo huku Bangladesh, ambapo wengi wa watu wa Rohingya wametorokea, serikali ziliamrisha kampuni za simu kufunga huduma za 3G na 4G katika kambi za wakimbizi za Rohingya na kusimamisha uuzajia wa kadi za simu Rohingya. Tunapoingia mwaka wa2020, miji minne ya Rakhine inaendelea kukosa kuunganishwa na ulimwengu, na Bangladesh inaendelea kuzuia huduma hizo katika kambi za wakimbizi.

Kuweka Nyaraka Wakati Mtandao Umezimwa

Duniani, kuzimwa kwa mitandao kumezidi. Kulingana na#Endeleza kampeni (#KeepItOn campaign) ya AccessNow’s, kulikuwa na visa 128 vya kusudi kati ya Januari - Julai 2019, kulinganisha na 196 mwaka mzima wa 2018, na 106 katika mwaka 2017, na 75 katika mwaka 2016. Kote ulimwenguni, serikali, kwa ushirikiano na kampuni za mawasiliano, zimekuwa zikizima mitandao kama njia ya kunyamazisha jamii, kuzuia uhamasishaji, na kuzuia tarifa za ukiukaji wa haki za kibinaadam kuandikishwa na kupokezanwa.
 

Kuzimwa mtandao na ukiukaji wa haki za kibinaadamu huenda bega kwa bega.”

- Berhan Taye, AccessNow

Kuzima huku kunawezachukua mifumo tofautitofauti,hii inajumuisha kufunga mifumo-fulani ambayo inalenga viunzi (apps) maarufu na tovuti, kuzimwa data za simu, kudhibiti vipimadata, aukuzimwa mitandao kabisa. Aina zote hizi za uzimaji mitandao zinalenga kuvuruga uwezo wa kuwasilisha taarifa na kuanika dhuluma na ukiukaji kwa wakati-halisi. TMara nyingi haya hutokea wakati wa maandamano, uchaguzi, na nyakati za migogoro ya kisiasa, na mara nyingi uandamana na ukandamizaji kutoka serikalini, mashambulizi ya kijeshi, na vurugu. Japokuwa serikali itajaribu kutetea uzimaji mitandao kisingizio cha “usalama wa taifa” au sababu nyinginezo, hakika kuzimwa huku hutokea wakati serikali dhalimu zinahofia kupoteza nafasi ya kudhibiti watu wake, taarifa, au maswala ya kisiasa. Uzimaji hukiuka haki za kibinaadamu, huvuruga  maisha na riziki za watu, na pia huwa na athari za kiuchumi ulimwenguni.
 

Kuweka nyaraka ya ukiukaji wa haki za kibinaadamu ni muhimu sana wakati wa kuzimwa kwa mtandao. Hata kama taarifa hazitapeanwa muda huo, kuweka nyaraka kutakuwa njia ya kuhifadhi sauti zile serikali zinataka kunyamazisha, na kuweka ushahidi wa dhuluma ambazo zitakuja kuwajibikiwa baadaye. Bila shaka, udhalimu, na vikwazo vya kiteknolojia vya kuzimwa kwa mtandao hufanya uwekaji nyaraka za ukiukaji – na kudumisha maelezo hayo kuwa salama– kuwa yenye changamoto na hatari. Ni vipi wanaharakati watanasa na kuhifadhi vidio zao wakati wa kuzimwa mitandao, na hata kupokezana vidio bila mtandao, na kufanya hivyo kwa njia salama? 

Msururu huu

Kupitia kazi yetu na wanaharakati ambao wamekumbana na uzimaji mtandao, tumejifunza vitu muhimu na jinsi ya kunasa na kuhifadhi nyaraka za vidio wakati wa kuzimwa kwa mtandao ambavyo tunapokezana kwenye msururu huu. Tuliwaandikia huku tukiwazia vifaa vya Android, japokuwa vidokezo hivyo vinaweza kutumika kwenye iPhones pia. Mikakati mingine inahitaji maandalizi ya mapema (na mara nyingi, kupata mtandao), hivyo basi ni wazo zuri kuhakiki na kutekeleza hatua zozote kabla ya kujipata katika mazingira ambayo hauna mtandao na unataka kuhifadhi maelezo. Weka nakala ya mojawapo ya mafundisho ambapo utapitia au kupeana  wakati wa kuzimwa mtandao.Na hatimaye, anza kujifundisha mbinu na njia kila shughuli zako za siku ili ziwe sehemu ya pili ya maisha yako kabla ujipate katika hali ngumu. 

Maelezo ya mwisho: Huku vidokezo hivi vitausaidia kuendelea kuweka nyaraka wakati huu wa kuzimwa mtandao, tungependa kusisitiza kuwa suluhu kamili ni kurudisha mtandao, na kupiganiahaki ya kurekodi, na uhuru wa kuongea, taarifa, na kujumuika. Kwa Bahati, kuna vuguvugu la ulimwengu likiongozwa na mashirika kamaNetBlocks, AccessNow, na mengine mengi ambayo yanaangalia na kupeana tarifa kuhusiana na uzimaji. Mawakili duniani wanatafuta mbinu mwafaka ya kisheria dhidi ya uzimaji mtandao.Tunawaunga mkono kweney kazi yao ya kutetea haki za kibinaadamu.
 

Naweza Kutumia Kiunzi Hiki Cha Nyaraka?

Mwisho iliangaliwa: 31 Januari 2020

Kuna viunzi vingi ambavyo waweka nyaraka wanaweza kutumia kunasa vidio, kuanzia kiunzi asili cha kamera, hadi kwa viunzi vya nyaraka spesheli zaidi kamaProofMode, Tella, auEyewitness to Atrocities. Viunzi vingine vina vigezo ambavyo vinategemea uwepo wa mtandao, hivyo kumbuka vigezo hivyo havitakuwepo wakati mtandao umezimwa. 

Hatuwezi kukuambia ni kiunzi kipi kinakufaa, kwa vile hiyo hutegemea na hali yako, mahitaji, na hatari, (angalia hili walisho kwenye blogu jinsi ya ni vipi unatathmini hatari na vitisho). Ukiwa na utathmini wa hatari, mwongozo huu maswali hapa chini utakusaidia kujua ni kiunzi kipi cha nyaraka za vidio ni bora kwako.
 

Ni nani alitengeneza kiunzi na nitawaamini? 

Tilia maanani mtengenezaji wa kiunzi chochote kile unapakua na kusakinisha kwenye simu yako, na iwapo unaweza kuwaamini ili usiwe hatarini, kwa kusudi au bila kusudi.

Baadhi ya vitu utazingatia ni:

  • Mtengenezaji wa kiunzi ana sifa nzuri? Ni nini watu wa jamii yako na walio karibu nawe wanasema kuwahusu na vifaa vyao?
  • Mtengenezaji yu hatarini? Zingatia sifa zao na uwezekano wao wa kulazimishwa kutoa data zako au kuweka mwanya wa serikali (au iwapo wamefanya hivyo awali). Ni nchi gani data zako zimehifadhiwa na sheria ni zipi kuhusiana na maagizo ya korti? 
  • Mtengenezaji wa kiunzi anakiboresha? Vifaa visivyoboreshwa viko hatarini kuvamiwa mtandaoni ambao wamegundua mwanya uliopo.Angalia tovuti ya mtengenezaji au kurasa za kiunzi hicho kwenye Google Play tarehe ya “mwisho uliandikwa/sasishwa.” 
  • Mtengenezaji kiunzi ameendelea kiasi gani, na wanaonekana watadumisha kiunzi hicho kwa muda mrefu? 
  • Kiunzi hicho ni huru? Viunzi vilivyo huru kudadisiwa vina uwezekano mkubwa masuala yao ya kiusalama kujadiliwa au angalau kutambuliwa. Je mtengenezaji una uwazi kuhusiana ubora na usalama wa kiunzi?
  • Ni motisha gani au vivutio vipi vindaendeleza kazi za mtengenezaji kiunzi, na ni vipi hilo litavutia uaminifu wao? Kwa mfano, je wana-lengo? Wanalenga-Faida? Wanafadhiliwa na mhisani fulani?
  • Huku hilo si ashirio la uaminifu au kama sivyo, bei ya kiunzi itakuwa ya muhimu kuzingatia. Viunzi vingine vina malipo ya juu ya kila mwezi au malipo ya kila vidio. 

Kwa habari zaidi Angalia EFF mwongozo wa uangalizi wa ulinzi-binafsi katika kuteua viunzi.
 

Ni kutoka wapi kiunzi kinapakuliwa?

Siku zote sharti upakue na kusakinisha viunzi kutoka  app stores au tovutizinazojulikana. Hata kama umefanya uchunguzi wa kina kuhusiana na kuaminika kwa kiunzi,hifadhi za viunzi zisizokamili zinaweza potosha kuhusu viunzi vyao na kusababisha kupakua haramu ambayo imetengenezwa kwa nia mbaya. Kwa mfano mwaka jana shirika la kupigania haki za mitandaoni SMEX ilitoa onyo kuhusu tovuti mbalimbali zilizokuwa zinatangaza kiunzi kinachoitwa “WhatsApp Plus” (kuweka mambo wazi, hii si bidhaa ya WhatsApp!), ambayo itakuwa ikihifadhi na kuuza data za mtumiaji, au kusababisha simu zilizokisakinisha kutapeliwa mtandaoni.

Baadhi ya watengenezaji walio makini na usalama utoa herufi za msimbo fiche ambazo zinakuruhusu kuthibitisha uhalali wake. Watatoa maelezo ya jinsi ya kuthibitisha sahihi hizo.
 

Ni wapi data zitahifadhiwa?

Baadhi ya viunzi vya nyaraka uhifadhi data na nyaraka kwenye simu yako, huku baadhi hutuma na kuhifadhi data kwingineko. Mara nyingi hii inasawiana na muundo na dhamira ya kiunzi, kama vile kiunzi cha Eyewitness to Atrocities, ambayo inatuma nakala ambayo haijabadilishwa ya nyaraka kwa hifadhi ya Lexis Nexis ili Eyewitness iweze kupigania ukweli wa maadili ya nyenzo. Unaweza kuhamisha vitu vyako kutoka hifadhi ya simu iliyosimbwa katika kiunzi cha Eyewitness baada ya kutumwa kwa ulinzi. 

Chaguo ni lako iwapo utaamua kuacha nyaraka kubaki kwenye simu yako pekee, ama unataka itumwe na kuhifadhiwa mbali ambayo utadhibiti (ambayo ni chaguo la Tella), au iwapo utahitaji kutuma kwenye mashirika ya nje / mfumo ambao utaruhusu kufikiwa na kutumia nyaraka zako. Kumbuka kuwa wakati wa kuzimwa mtandao, huwezi kutuma nyaraka zako mtandaoni wakati huo huo, hivyo utahitaji kiunzi ambacho kitakurusu angalao kwa muda uhifadhi (na kuimarisha) nyaraka zako eneo lako (AngaliaKuimarisha data  za simu bila mtandao au tarakilishi).

Iwapo data zako zitatumwa eneo la mbali, fahamu nchi ambayo data zako zitakuwa. Kuna hatari gani ya data zako kufichuliwa katika hizo nchi, iwapo ni kupitia maagizo ya korti au namna nyingine? Ni hatari zipi utapata data zako zikifichuliwa huko?
 

Je kiunzi usimba/kuficha taarifa zangu?

Baadhi ya viunzi, kama Tella na Eyewitness to Atrocities, huwa na msimbo fiche wa faili au na / au hifadhi iliosimbwa kwa nyaraka zako, kando na hifadhi ya simu yako na msimbo fiche wa simu, ili taarifa na datajumla za simu yako hazitawahi kusimbwa kwenye simu yako hadi ifikiwe kwa kutumia kiunzi yenye pasikodi. Hii inamaanisha kuwa hata kama simu yako imefunguliwa, nyaraka zako zimesimbwa. Hii inatoa viwango vingine vya usalama kwa uwekaji nyaraka zako.

Iwapo kiunzi kitatuma na kuhifadhi taarifa zako eneo la mbali baada ya mtandao wako kurudishwa, pia fikiria iwapo unahitaji taarifa zako zisimbwe zikiwa njiani na zikiwa eneo la mbali, kwa mfano vile kiunzi cha EyeWitness hufanya.

Kumbuka kuwa huku usimbaji fiche ni halali takribani kila eneo, baadhi ya nchi huenda zina sheria ambazo huzuia au kuharamisha matumiazi yake. Hii ramani (ya jumla, lakini ya kutoka mwaka 2017) inatoa mwelekeo mzuri iwapo una maswali kuhusiana na sheria za nchini mwako.
 

Je Kiunzi kinanasa dataelezi (bila mtandao)? 

Dataelezi nidata ambazo huelezea vidio au picha yako, kama vile wakati na tarehe au eneo. Hii taarifa ni muhimu kwa kutambua, kuelewa, uhalisia, na kuthibitisha vidio au picha kama nyaraka za wakati fulani.Wakati wa mtandao kuzimwa, uwezo wa kiunzi kukusanya dataelezi Fulani moja kwa moja na/au kukuruhusu kwa urahisi kuweka taarifa fafanuzi papo hapo ni ya kufaa sana, kwa vile kuna muda mrefu kabla ya kupokezana nyaraka na yeyote (wakati ambapo maelezo yatakuwa yamesauhulika, hali kubadilika, nk, nk). 

Nyingi ya viunzi spesheli vya nyaraka kama vile ProofMode vina vigezo bora vya dataelezi, na ukusanya dataelezi nyingi kuliko kiunzi cha kamera ya ndani. Dataelezi bora hujumuisha data za sensor, au wifi au viashiria vya bluetooth, data za simu, kipimo chakripografia, na taarifa ilisambazwa kwa mtumiaji, ambapo zote zinawezesha uhalisia na uthibitisho wa taarifa baadaye.

Kumbuka kuwa wakati mtandao umezimwa, utahitaji kiunzi ambacho hakitaki data ili kutoa au kurekodi dataelezi. Baadhi ya viunzi vitategemea mtandao, badala ya vifaavya sense, kukusanya dataelezi Fulani. Mfano, iwapo data za eneo zimenaswa kupitia mpangilio wa simu, dataelezi huenda zikaangazia eneo la mwisho ambalo simu ilikuwa na mtandao, badala ya mahali halisi pa kifaa. Kiunzi pia kinafaa kukurusu kuhifadhi dataelezi zako katika eneo lako bila mtandao, ikijumuisha kuhifadhi fomu ambazo unajaza (k.v. Tella’s “hali ya bila mtandao”).
 

Ninaweza hamisha data kutoka kwenye kiunzi?

Kutegemea na nia yako ya kuweka nyaraka, itakuwa inafaa kuhamisha nyaraka za vidio na dataelezi kutoka kwenye kiunzi, kwa mfumo ambao si umiliki wa kiunzi; yaani, utaweza kufungua, kuona, na kutumia taarifa na dataelezi nje ya kiunzi. Uwezo wa kuhamisha inamaanisha kuwa wewe na wengine hamtegemei kiunzi kimoja au mtoaji huduma ili kufikia nyaraka zako, na inakupa nafasi kubwa kufanya kazi zako kuendelea mbele. Kumbuka kuwa baadhi ya dataelezi hazieleweka kama hauna datamsingi au chati kufafanua nambari (kwa mfano, kama utambulisho wa mnara au mitandao ya Wi-Fi networks). 

Kumbuka baadhi ya viunzi vina msururu wa uangalizi uliofungwa kusudi na hauruhusu watumiaji kuhamisha, huku baadhi ya viunzi havichaundwa kwa kusudi la kuhamisha. Pia jua kuwa baadhi ya viunzi kama Eyewitness to Atrocities, havitakuruhusu uhamishe hadi upakia taarifa zako kwenye sava ya mbali (ambayo unahitaji mtandao ili kufanikisha), na baadhi ya viunzi vitakuruhusu kuhamisha taarifa, lakini si dataelezi (mbali na dataelezi zilizo kwenye faili binafsi).

Iwapo unataka kuhamisha, kimsingi kiunzi chako sharti kikuruhusu kuhamisha nakala ya taarifa bila mabadiliko yoyote au umbuaji, na nakala ya dataelezi ikiwa katika mfumo wastani unao maandishi ya kusomeka. Kwa mfano dataelezi ya Tella, inahifadhiwa kwenye na kufichwa katika hifadhi ya Tella, lakini yaweza kuhamishwa kama CSV. Pia, wakati mtandao umezimwa, ni muhimu kuwa na njia mbadala ya kuhamisha kwenye viunzi visivyio na mtandao au huduma zisizotegemea-mtandao. Idadi kubwa ya viunzi vinavyokuruhusu kuhamisha vina kitufe cha “Pokeza” ambayo inachochea menyu ya upokezanaji, ambayo Android imejaza orodha ya viunzi katika simu yako ambavyo vina uwezo wa kushughulikia aina kama hiyo ya kazi. Bahati mbaya watengenezaji wa viunzi wanaweza kuunda menyu yao ya upokezanaji na hamna mfululizo baina ya viunzi. 

Kwa idadi kubwa ya faili, itakuwa vizuri zaidi kufikia faili zilizohifadhiwa kupitia kiunzi simamizi za faili na kunakili faili kutoka hapo, japokuwa hautakuwa na uwezowa kufikia dataelezi zilizohifadhiwa katika datamsingi za kiunzi namna hii. Chaguo hili pia halipo kwa viunzi ambavyo hujisimamia hifadhi zao salama, kwa vile faili zitafichwa katika ghala ya simu. Kwa viunzi hivi, ni vizuri kuwa na kiwezeshi cha kupokezana katika kiunzi.

Angalia chati yetu ya ulinganisho ya viunzi vya uwekaji nyaraka, na walisho lijalo kwenye msururu huu, “Kudumisha Taarifa Zilizothibitika Wakati Mtandao Umezimwa.”

*************************************************************************************************************

Kudumisha Taarifa Zilizothibitika Wakati Mtandao Umezimwa

Hili wasilisho ni sehemu ya msururu kwenye Kuweka Nyaraka Wakati Mtandao Umezimwa.

Ilingalaliwa mwisho: 31 Januari 2020

Watetezi wa haki za kibinaadamu, mpelelezi, watafiti, na wanahabarimara  nyingi hutegemea nyaraka za mwanzo ambazo zilinaswa filamu na mashahidi kufanya uangalizi, kuripoti, na kuongolelea ukiukaji wa haki za kibinaadamu. Ili kuhakikisha kwamba wanapiga hatua kwakutumia taarifa sahihi, watumiaji hawa hupiga hatua kutafuta uhalali na kuthibitisha nyaraka wanapokea, mchakato ambao una machungu na hutumia-muda mwingi.

Kama mweka nyaraka, kuna vitu kawaida utafanya ili kurahisishia wengine kuthibitisha na kukubalia nyaraka, ili kutumiwa kwa muda na njia zifaazo. Hizi hatua chache ni muhimu zaidi wakati mtandao umezimwa, ukizingatia kuwa:

  • Kama hautapakia papo hapo,, tarehe ya uchapishaji na taarifa ya eneo inatolewa katika mitandao ya kijamii haisaidii kwa kuonyesha kuwa vidio yako ilinaswa tarehe au kabla ya tarehe Fulani au katika eneo Fulani.
  • Iwapo wengine hawapakia labda, huenda kuwe uwekaji nyaraka uliopungua kwa jumla ambao utatumiwa kukubalia vidio yako.
  • Iwapo unataka vidio yako ipitie hatua kadhaa bila mtandao ili ifike inalenga, inaweza kuwa vigumu kwa wengine kufuatilizia mwanzo wa vidio hiyo.
  • Iwapo unataka kufuta vidio asilia kutoka katika simu yako kwa sababu ya usalama au nafasi kidogo ya uhifadhi ambao hauna mtandao imara, au iwapo unataka kutupa simu yako, huenda iwe vigumu kuthibitisha uhalali wa vidio. 
  • Iwapo umesahau maelezo kuhusu vidio Fulani na kiunzi unachotimia hakinasi / kurekodi dataelezi bila mtandao, wengine hawataweza kuitambua baadaye.

Vidokezo vifuatavyo vitakusaidia kudumisha vidio yako wakti mtandao umezimwaili kuchukua nafasi ya uhalali wake na utumiaji kuwa nyaraka zako baadaye.

Nasa au toa maelezo ya kutambua vidio

Jaribu kujuisha maelezo katika vidio yako ambayo yatamrahisishia mpelelezi au mwanahabari baadaye kutambua wakati na eneo, kama vile upekee wa maeneo, anga, alama za mitaani, maduka makuu, mabamba ya leseni, bendera, saa, kurasa za mbele za gazeti, nk. Unaweza pia ukasimulia taarifa muhimu kama vile jina lako, na taarifa za mawasiliano (iwapo ni salama kufanya hivyo), wakati, tarehe na eneo/GPS inashirikiana (au andika kwenye karatasi na nasa hiyo karatasi). Unapotoa maelezo mengi, hivyo ndivyo rahisi itakuwa kwa mtu mwengine kutafiti na kuthibitisha vidio baadaye, hata kama hawakujui au ni wapi vidio ilitoka. Angalia vidokezo vyetu kwenye Mafunzo ya Kimsingi yaKunasa, Kuhifadhi na Kupokezana kwa mengi zaidi.

Ongeza maelezo / dataelezi 

Chukua nafasi ya pekee kupata moja ya viunzi spesheli vya nyaraka ambavyo uweka dataelezi bora au taarifa za kiufundi kutoka katika simu yako, na kukuruhusu kuweka taarifa za maelezo ziada kwa njia ya kawaida. Kumbuka kwamba, wakati wa kuzimwa, unahitaji kiunzi ambacho hakitegemei mtandao ili kurekodi au kuhifadhi dataelezi. Angalia“Ninaweza Kutumia Kiunzi Hiki cha Nyaraka?Kwa habari zaidi jinsi ya kuchagua kiunzi kinachofaa.

Hata kama hutumii kiunzi spesheli cha nyaraka, unawza bado kutengeneza taarifa za ziada kwa njia ya mukhutasari, ramani, au picha katika simu yako. Unaweza panga simu yako na taarifa hii ya ziada ukitumia kiunzi angalizi anachopendelea. Taarifa muhimu za ziada ni pamoja na , wakati, tarehe, eneo kulikorekodiwa kisa, vilevile mwanzo/chanzo cha rekodi hiyo. (h.n.kjina lako na maelezo ya mawasiliano) iwapo ni salama kujumuishwa. Hamisha dataelezi na jumuisha na vidio (zote ziweke kwenye kabrasha na ufunge) wakti unapokezana.

Weka Akiba 

Weka akiba ya taarifa zako kutoka katika simu yako kila mara, hasa kwenye hifadhi 2 za simu. Unaweza, kwa mfano, kuunganisha kwenye On-the-Go (OTG) au flashi kwenye simu yako, hata bila tarakilishi. Angalia vidokezo vyetu kwenye “Kuweka akiba taarifa simu bila mtandao au tarakilishi” kwa maelezo zaidi. Kuweka akiba itahakikisha kwamba unabaki na nakala ya video yako iwapo utapoteza au simu yako ivunjike, au unataka kufuta vidio kutoka simu yako. Kuwa na nakala asili iliyo salama pia inamwezesha mpelelezi au mwanahabari ambaye atakuwa ameona vidio yako kupitia mianya mingine kupata iyo vidio moja kwa moja kutoka kwako baadaye (mradi wanaweza kuifuata hadi kwako), kuandaa msururu wa usimamizi uliomfupi na uliokamilika.
 

Angalia wasilisho lijalo katika msururu huu, “Kuweka Akiba Ya Taarifa Ya Simu Bila Mtandao au Tarakilishi.”

*************************************************************************************************************

Kuweka Akiba Ya Taarifa Ya Simu Bila Mtandao au Tarakilishi.

Hili wasilisho ni sehemu ya msururu kwenye Kuweka Nyaraka Wakati Mtandao Umezimwa.

Ilingalaliwa mwisho: 31 Januari 2020

Kuweka Akiba ni muhimu kwa kuhakikisha kuwa data na nyaraka hazifutwi kwa bahati mbaya, kuharibika, au kupotea iwapo simu yako imenyakuliwa. Wakati wa mtandao umezimwa au kujikokota huenda usiweze kuendesha uwekaji akiba wako wa kila mara au kutuma nyaraka zako katika eneo la mbali lililo mbali.Kuweka katika tarakilishi au kipakatalishi ni njia moja ya kuweka akiba, kwa vile watu mara nyingi hawana njia ya kupata tarakilishi,  hapa kuna baadhi ya chuguo na vidokezo vya kuweka akiba ya taarifa kutoka simu yako wakati wa mtandao umezimwa na hauna tarakilishi. 

Tumia OTG au flashi 

OTG, au on-the-go, flashi ni aina ya USB ambazo zinawiana na nyingi ya Androids(lakini si zote). Unaweza kuunganisha flashi ya OTG moja kwa moja kuenda simu yako, au utumie adapta ya OTG-kuenda-USB kuunganisha simu yako kwa USB ya kawaida. Kuhusu OTG, simu yako itatoa kawi kwayo.

Bidhaa maarufu za flashi za OTG ni pamoja na SanDisk, Kingston, na Samsung, japokuwa kuna nyinginezo. Kawaida zinagharimu US$8-$25 kutegea na uwezo wa kuweka. Flashi zisizochomekwa / flashi kubwa ni sawa na flashi kawaida za kawaida ila hazihitaji waya. Hii itakuruhusu kuunganisha kwenye simu ambazo kawaida haziunganishi kwenye flashi, kama vile simu yako. Umuhimu waflashi isiyochomekwa dhidi ya ya flashi ya OTG drive ni kwamba unaweza kuunganisha vifaa vingi kwenye flashi hiyo kwa wakati mmoja.Hii itakuwa ya msaada, kwa mfano, katika maandamano ambapo wakati unanasa filamu kama kikundi –picha ya kila mmoja itawekwa akiba kwnye flashi ambayo wenzao watakuwa wamebeba. Kumbuka kuwa kwa sababu hazitumii kawi kutoka kwenye simu, flashi zisizochomekwa zinategea kawi ya betri na zinafaa kuchajiwa.

SanDisk ndio labda bidhaa maarufu ya flashi zisizochomekwa, japokuwa kuna nyingine. Flashi zisizochomekwa ni ghali zaidi kuliko flashi za OTG ,na zinaanzia kutoka  US $25-$100 kutegemea na uwezo wa viwango vya kuhifadhi. Flashi zisizochomekwa kubwa zinaanzia US$150 uwezo wa viwango vya kuhifadhi.

Njia mbadala: Tumia simu zee ambayo haitumiki

Iwapo hauna OTG au or flashi isiyochomekwa, lakini una simu zee ambayo bado inafanya na hauitumii, unaweza pia kuitumia kuweka akiba. Mradi  simu zote ziko katika umbali wa kukaribiana, unaweza kuunganisha na kunakili taarifa kutoka moja kuenda kwa nyingine ukitumia Bluetooth, WiFi Direct, au Near Field Communication (NFC) / Android Beam. Bluetooth na Wifi Direct zote ni teknojia zisizochomekwa ambazo zita“kuunganisha” simu mbili bila kiunganishi cha mtandao (router) au kitovu cha kuunganisha mtandao baina yazo. WiFi Direct utoa nafasi pana na data za kasi ya juu za kuhamisha kuliko Bluetooth, lakini utumia kawi nyingi. Hata hivyo, NFC ina nafasi ndogo (~4cm) na kasi ya chini ya kuhamisha kuliko Bluetooth au WiFi Direct, lakini ujiunganisha haraka na hutumia kawi kidogo, hivyo inaweza kuwa ya manufaa kwa uhamishaji wa haraka wakati una simu zote mkononi.

Simu yako labda ina Bluetooth ya ndani, WiFi Direct, au viunzi vya NFC / vigezo ambavyo vinakuruhusu kuchagua simu iliyo karibu ili kupokezana nayo. Iwapo simu zote zina Files By Google ambazo zimesakinishwa, unaweza pia kupokezana faili bila mtandao ukitumia teknolojia hii kwenye kiunzi. 

Muhimu: ubaya wa uunganishaji huu wa rahisi ambao unatolewa na huduma hizi ni haupo salama. Bluetooth naviashiria vya wifi /midaki inaweza kutumika kufuata eneo uko au kuchunguza taarifa katika simu yako. Matapeli wanaweza kujaribu kuunganisha simu yako, wakutumie faili hauhitaji, au wapate nafasi ya kudhibiti simu yako iwapo hatarini.Ili kuwa salama, funga huduma hizi wakati hauzitumii na iwashe tu wakati uko katika maeneo salama, fanyakiunzi chako kukubali tu kile unacho/Yule unamhitaji, na tekeleza usalama wa simu uliobora kama vile kuendeleza usasishaji na kuwa na pasikodi imara.

Jumuisha maelezo ya kando yoyote / dataelezi

Wakati unanakili taarifa kuenda katika flashi ya OT, flashi isiyochomekwa, au simu zee, ni vizuri kujumuisha taarifa za kuelezea au dataelezi ambazo zitakuwa kando na taarifa. Nyingi ya viunzi vya nyaraka, kwa mfano, hutoa nyaraka za maandishi za CSV au JSON ambazo hujumuisha dataelezi ambazo zimetolewa kutoka kwenye simu (k.v. jeografia ya eneo, wakati, tarehe) na maelezo yoyote yaliyowekwa na mtumiaji kwa njia ya kawaida. Hakikisha kwamba unahamisha na kujumuisha hizi nyaraka za dataelezi kwenye akiba yako pia.  

Nywila hukinga flashi

Nyingi ya flashi zisizochomekwa zinawezwa kingwa-na nywila na kiunzi cha simu ambacho kinakuja na flashi. Kumbuka kuwa ukingaji ukitumia-nywila si sawa na usimbaji fiche (ona hapo chini). Nyingi ya flashi zisizochomekwa au za OTG haziweziruhusu usimbaji kamili-wa-diski kwa kutumia simu ya rununu tu, japokuwa zinaweza ruhusu usimbaji kalmilifu wa diski kwa kutumia tarakilishi.

Zingatia kusimba faili

Iwapo unataka kuhifadhi faili zako salama aidi, unaweza kuzingatia kusimba akiba zako.Huku hautaweza kusimba nyingi ya flashi zisizochomekwa au za OTG ukitumia simu ya rununu, unaweza kusimba faili kabla haujazihamisha katika flashi. Baadhi ya viunzi ambavyo vinasimba faili katika AndroidniZArchiver, na RAR. Kumbuka kuwa sharti ukumbuke nywila yako ya usimbaji.Hakuna njia ya kupata faili zilizosimbwa iwapo utasahau nywila.

Kumbuka baadhi ya nchi huenda zina sheria ambazo zinazuia au zinaharamisha matumizi ya viunzi vya usalama wa simu ambavyo uficha au kufuta data zako. Kuvitumia kuzuia serikali kuangalia data zako inaweza kuchukuliwa kuwa inaharibu ushahidi au kutatiza uchunguzi, na inaweza kuadhibiwa kama ya uhalifu. Hii ramani (ya jumla, lakini ya kutoka mwaka 2017) inatoa mwelekeo mzuri iwapo una maswali kuhusiana na sheria za nchi.

Unda akiba 2 kwenye maeneo tofauti 

Akiba moja kamwe haitegemeki.Kwa mfano, unaweza kupoteza simu ya akiba, iharibike, au inaweza kufeli. Wataalamu wa teknolojia wanashauru watu kuwa na akiba 2 (yaani nakala 3 kwa jumla), kawenye simu tofauti zilizo katika maeneo tofauti.  Hii inasaidia kupunguza nyingi ya hatari kwenye nakala yoyote yazo.

Angalia wasilisho la mwisho katika msururu huu, “Upokezenaji Wa Faili na Mawasiliano Wakati Mtandao Umezimwa.”

*************************************************************************************************************

Upokezenaji Wa Faili na Mawasiliano Wakati Mtandao Umezimwa 

Wasilisho hili ni sehemu ya msururu kwenye Uwekaji Nyaraka Wakati Mtandao Umezimwa.

Mwisho iliangaliwa: 31 Januari 2020

Uzimaji na ukataji wa mtandaounaoendelea Kashmir, uzimaji wa mtandao ulioendelea kwa muda mrefu zaidi ambao umewekwa kwa nchi, umekuwa na athari mbayakwa maisha ya watu katika ukanda huo. Kuongeza machungu kwenye kidonda, Disemba 2019, akauntiza WhatsApp raia wa Kashmiri zilianzakubatilishwa kutokana na watumiaji kukosa kutumia akaunti zao kwa siku 120 kulingana na sera za WhatsApp.

Wakati wa kuandika haya mwezi Januari 2020, Mahakama ya Juu ya India iliamua kuwa uzimaji mtandao huko Kashmir ni kinyume cha sheria na matumizi mabaya ya mamlaka. Mtandao wa kasi na ule wa simu umerudishwa kwa baadhi ya maeneo, lakini unachagua tovuti “zilizotengwa” tu.

Uzimaji mtandao unalenga kuwazuia watu kupokezana taarifa na mawasiliano (na pia kulazimisha watu kuwa katika hali ya mawasiliano duni kama vile simu na Jumbe Fupi, ambayo ni rahisi kwa serikali kuingilia na kufuatilizia). Kamwe hamna mbinu nzuri ya suluhu wakati mtandao umezimwa kabisa.Wakati wa mgumu zaidi wa uzimaji Kashmir, kwa mfano, watu waliamua kutumia maandishi na huduma za barua ili kufikisha ujumbe kwa wapendwa wao. 

Hatuna njia ya uhakika ya kufaulu kwenye kufungwa kote huku, lakini kupitia mazungumzo na wanaharakati na washirika, tumejifundisha baadhi ya mbinu na njia za kutumia kwa upokezenaji bila mtandao na mawasiliano ambayo yatakufaa wewe, kutegemea na hali. Kumbuka kwamba baadhi ya njia hizi uhitaji mtandao ili kutekelezeka (k.v kupakua viunzi, n.k).
 

Pokezana faili moja kwa moja ukitumia Bluetooth, Wifi Direct, au NFC 

Hauhitaji mtandao ili kunganisha simu yako na kifaa kingine cha karibu kutumia Bluetooth, Wifi Direct, au Near Field Communication (NFC) (mara nyingine huitwa Android Beam kwenye simu za zamani). Bluetooth na Wifi Direct zote ni za teknolojia ambazo hazichomekwi na zina uwezo wa “kuunganisha” simu mbili bila ruta au kiunganishi baina yazo. WiFi Direct inatoa nafasi pana na kasi ya juu ya uhamishaji data kuliko Bluetooth, lakini inatumia kawi nyingi. NFCina nafasi fupi (~4cm) na kasi ya chini ya kuhamisha kuliko Bluetooth au WiFi Direct, lakini uunganisha haraka na hutumia kawi kidogo, hivyo basi inaweza kuwa ya manufaa katika uhamishaji kidogokidogo wakati una vifaa vyote mkononi.

Bila shaka una vigezo vya Bluetooth, WiFi Direct, na NFC ambavyo vimeundwa kwenye simu yako ambavyo vinajitokeza katika chaguo zako za kupokezana. Na zaidi, viunzi venye faili zenye vigezo vya kupokezana, kama Files By Google, pia changanya teknolojia hizi.

Muhimu: ubaya wa uunganishaji huu wa rahisi ambao unatolewa na huduma hizi ni haupo salama. Bluetooth na viashiria vya wifi /midaki inaweza kutumika kufuata eneo uko au kuchunguza taarifa katika simu yako. Matapeli wanaweza kujaribu kuunganisha simu yako, wakutumie faili ambazo hauhitaji, au wapate nafasi ya kudhibiti simu yako iwapo uko kwenye hatari.Ili kuwa salama, funga huduma hizi wakati hauzitumii na iwashe tu wakati uko katika maeneo salama, fanya kiunzi chako kukubali tu kile unacho/Yule unamhitaji, na tekeleza usalama wa simu uliobora kama vile kuendeleza usasishaji na kuwa na pasikodi imara.
 

Kupokezana faili kwa flashi isiyochomekwa au kupitia Mtandao wa Eneo Lako (WLAN)

Flashiisiyochomekwa au flashi ya kuchomekwa inaweza kutumika kupokezana faili miongoni mwa kundi, au watu wengi kwa wakati mmoja. Kifaa cha wifi kitakuwa namaagizo na/au kiunzi cha kuunganisha simu yako kwenye kiunganishi, na rahisi kutumia.Kumbuka kuweka nywila kwenye kiunganishi kwa sababu ya kiusalama. 

Kama hauna flashi isochomekwa, unaweza pia kupokezana faili ukitumia flashi ya kawaida USB kwa kuweka kwenye ruta isiyochomekwa. Ruta ya kubebeka yenye kisimo cha USB, kwa mfano, si ghali na inabebeka. Watumiaji wanaweza kuunganisha kwa flashi ya USB kupitia mtandao wa eneo lako (mtandao hauhitajiki). Ili kupata faili katika flashi ya USB ambayo imeunganishwa kwenye simu yako, utahitaji kutumia kiunzi kisimamizi cha faili ambacho kitakuunganisha kwenye hifadhi iliounganishwa, kama vileSolid Explorer. Anwani ya IP ya ruta itapatikana kawaida katika mpangilio wawifi wa simu yako. 

Pia, chaguo jingine niPirateBox, jifanyie-wewe-binafsi mradi ambao unatoa kiunzi cha leseni bure. Watumiaji wanaweza pokezana faili jinsi inavyosema hapo juu, lakini Piratebox inawaruhusu kutekeleza bila kujulikana, na pia hujumuishavigezo vya kuchati na jumbe.Kuweka Piratebox inahitajikupakua, kusakinisha, na kuweka baadhi ya viunzi. Maagizoyako kwenye tovuti ya Piratebox.

Sasisha: mradi waPirate Boxunaelekea kuisha. Tovuti naeneo github vipo mtandaoni, lakini mwanzilishi mkuu wa mradi haihudumii kikamilifu.

Wasiliana kupitia chati peer-to-peer 

Viunzi vya kutuma jumbe viwili vipia vya peer-to-peer ambavyo tumejua kupitia miungano ya wanaharakati niBriarnaBridgefy. Hatujavijaribu bado, lakini tunajua wengine ambao wanavijaribu.

Briarni chanzo huru, kiunzi cha jumbe zilizosimbwa za moja kwa moja ambacho hakitegei sava kuu, badala yake sawazisha jumbe baina ya simu zawatumiaji(kwa hivyo kazi zao zinakaa katika simu ya kila mtumiajia). Inaweza kusawazisha hata wakati hamna mtandao kwa kutumia Bluetooth au WiFi (wakati kuna mtandao, viunzi husawazisha simu kutumia angavu zaTor). Briar pia huwa na makundi binafsi, makongamano ya adhara, na blogu.Unapotumia bila mtandao, nafasi yako imetegemea nafasi ya Bluetooth au WiFi (vipimo vya juu ~ mita 100).

Bridgefyni kiunzi cha moja kwa moja (ila wakati unatumia kigezo “sauti”) cha jumbe kilichosimbwa  ambacho hutumia Bluetooth kutuma jumbe. Kinyume naBriar, jumbe zinaweza enda mbali kwa kupitia miundo ya angavu ya watumiaji wengine wa Bridgefy (mlengwa wa ujumbe ndiye pekee atakayesoma ujumbe). Bridgefy inakosa makundi binafsi, makongamano, na blogu vya Briar, lakini kina kiwezeshi cha Sauti kupitia kwayo ambako utaweza kutuma jumbe kwa watumiaji 7 wa Bridgefy walio karibu, ambao hawahitaji kuwa kwenye mawasiliano yako (Jumbe za Sauti hazina lazima ya kusimbwa).

Wasiliana kupitia Ujembe uliosimbwa

Jumbe fupi hutumwa kupitia mitandao simu na haitegemei mtandao, kwa hivyo itafanya bado hata wakati mtandao umezimwa. Hata hivyo jumbe fupi zinaaminika kuwa hazina usalama. Kinyume na viunzi tegemezi vya mtandao kama vile WhatsApp au Signal, jumbe fupi hazisimbwi moja kwa moja. Hii inamaanisha jumbe fupi (na dataelezi zao) zinaweza kusomwa na serikali na mashirika ya simu, au kuvamiwa na matapeli wa mtandaoni. Jumbe fupi pia zinaweza “laghai,” kumaanisha anayetuma jumbe anaweza kutumia ujanja wa taarifa ya anwani yake na kujifanya mtumiajia mwengine.

Iwapo unataka kutumia Ujumbe mfupi, Silence ni kiunzi ambacho usimba jumbe za moja kwa moja. Ni chanzo-wazina inatumia utaratibu wa usimbaji wa Signal. Huku ikiwa sisi hatujakijaribu, tumesikia wengine wamekitumia. Mtumaji na mpokeaji wote wanafaa kukisakinisha na kubadilishana nywila nyinyi kwa nyinyi. Kwa vile jumbe fupi lazima huwa yapitia kwenye sava za shirika la mawasiliano, hata kwenye Silence ukizingatia kwamba unatuma jumbe zilizosimbwa na dataelezi kuhusu jumbe zako zitapitiwa na shirika la mawasiliano. 

Uzimaji baadhi wa mtandao: Kusuluhisha tovuti zilizofungwa

“Uzamaji mtandao” haimanishi kuzima kabisa, ila ni kufunga ufikiajia baadhi ya tovuti Fulani au mifumo ya mitandao ya kijamii. Serikali, kupitia watoaji huduma za mtandao (ISPs), inaweza kufunga tovuti kulingana na anwani ya IP, kazi zako, au kupitia DNS. Hauna uhakika kama tovuti yako imefungwa? Mashirika kama Open Observatory of Network Interference na Netblocks uangalia na kupima uvurugaji wa mtandao na ukataji ulimwenguni. 

Kwa Bahati nzuri, mradi unao mtandao, kuna baadhi ya njia utajaribu kusuluhisha uzimaji kwa baadhi. Kuhusu usimbaji, kumbuka kuwa kusuluhisha tovuti zilizofungwa zinaweza kuharamisha katika nchi yako.Fortunately, as long as you have internet access, there are some ways to try to get around the partial blocks. As with encryption, keep in mind that circumventing blocked sites may be criminalized in your country.
 

VPN

Njia moja ya kuweka nafasi mbadala ya kuleta suluhu kwa uzuiaji wa IP na uzuiaji wa kazi zako ni kutumia angavu binafsi za mtandao VPN, kama vile ProtonVPN au TunnelBear. Unapounganisha kupitia VPN, mvuto wa mtandao unasimbwa na kuunganishwa kupitia sava ya VPN katika eneo jingine, kama vile katika nchi nyingine, hivyo kuficha mwelekeo halisi na kilichomo katika mvuto kuelekea ISP.

Kumbuka kwamba baadhi ya serikali zimepiga marufuku matumizi ya VPN au zinaweza kujaribu kuchunguza na kuzuia unganishaji wa VPN. Ni muhimu pia kutumia watoaji wa VPN wanaoaminika, na hasa ile ambayo haiwezi kuhifadhi data au logi, kwani mtoaji huduma atakuwa anaona shughuli zako za mtandaoni. Fahamu mtoaji wa VPN anatoka nchi gani, na ni mchakato upi wa kisheria watatumia kulingana na mamlaka yao. Pia kumbuka VPN zilizothibitishwa na serikali zinawezesha uangalizi na ukaguzi wa data zako. 

Sava za DNS 

DNS (“mfumo wa jina la kikoa”) sava ufanya kazi kwa kutafsiri majina ya kikoa au URL ambayo mtumiaji anaandika kwenye kivinjari hadi kwenye anwani za nambari za IP ambayo mtandao unatumia kutambua kurasa za tovuti. ISP ina weza kubadilisha sava ya DNS inadhibiti kuzuia baadhi ya maswali, au kurudisha kurasa isiyo sahihi na kusema tovuti husika haipo. Mwaka 2014, Waziri Mkuu wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan alijaribu kufunga Twitter wakti wa uchaguzi mkuu nchini humo akitumia mbinu hii. Marufu hayo yalizuiwa kwa haraka na wanaharakati ambao wapokezana vidokezo hatua-kwa-hatua jinsi ya kutumia VPN na kubadilisha sava za DNS. 

Unaweza kubadilisha sava msingi za DNS katika angavu za simu yako au mpangilio wa wifi. Badala ya sava msingi ya DNS, unaweza tumia sava mbadala za DNS kama Google Public DNS au CloudFlare ili kusuluhisha uzuizji wa DNS. Cloudflare pia ina kiunzi kinaitwa1.1.1.1 ambacho kinaruhusu watumiaji kuingia sava ya Cloudflare DNS kupitia mfumo wa kiunzi. 

Hizi tu njia mbili za kuzuia mbinu zinazotumika sana katika ufungaji mitandao. Angalia miongozo muhimu kutoka Internet Society, Access Now, Security-in-a-Box, na EFF kwa taarifa za kina zaidi.

Kozi zinazohusiana

  • 60 dakika

    Shutdown Academy

    Kichwa cha Kosi : Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao

    WITNESS

    60 dakika

    WITNESS
  • Open Observatory of Network Interference (OONI)

    90 dakika

    Open Observatory of Network Interference (OONI)

Zanakazi

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
  • Faragha
  • Maagizo