Tunafurahia kutangaza uzinduzi wa tovuti yetu mpya!
Miezi michache iliyopita, tulianza safari ya kutafakari tovuti yetu kuangazia uvumbuzi wa kazi yetu. Tovuti yetu mpya ina muundo mzuri na kontenti za kuelemisha ili kukusaidia kufahamu kutuhusu, kozi zetu, na nyenzo zetu.
Tuanze na Lengo Kuu: Tunaleta kwenu Mwonekano wetu Mpya!
Tovuti ya Advocacy Assembly ina mwonekano mpya. Kundi letu limekuwa ikimakinikia matumizi yaliyo rahisi kwa mtumiaji ili kuweka hatua ya mafundisho yako katika viwango vingine.
Advocacy Assembly katika Kifaransa, Kireno na Kiswahili
Tunafurahia kupiga hatua hii kwa kufanya Advocacy Assembly kupatikana na ya kutegemewa na mtumiaji kwa wanajamii wetu mbalimbali. Kuanzia leo, Advocacy Assembly inapatikana katika Kifaransa, Kireno na Kiswahili.
Iwapo unataka kupitia kozi zetu, jifunze kutokana na nyenzo zetu, au soma makala yetu, unaweza kufanya hivyo sasa katika lugha unayopendelea. Wataalam wetu wa lugha na watafsiri wamefanya kazi kwa bidii kuhakikisha kuwa kontenti si tu kuwa shwari vilevile inakuwa na uhalisia wa nyenzo lengwa.
Ili kuweka katika lugha yako, bofya katika kitufe cha lugha kilichoko juu ya ukurasa na teua lugha unayopendelea.
Zanakazi Mpya kwa Zinapatikana
Tunafurahia kuleta kitengo kipya cha tovuti yetu ambacho kitakupa taarifa muhimu kwa kina. Pitia kitengo chetu kipya: Zanakazi!
Zanakazi ni nyenzo zimeundwa kwa umakini ili kukupa ufahamu, maagizo ya kila hatua, na vidokezo vya watalaam kwa mada mbalimbali zinazohusiana na haki za kidijitali na zaidi.
Uko Tayari? Kwa Namna Hii:
Pita hadi kwenye "Zanakazi" kitengo chini ya “Nyenzo” kutoka katika menyu kuu.
Pita katika mkusanyiko wetu wa zana unaoendelea kupanuka unaangazia mada mbalimbali
Bofya katika zanakazi ambayo utapendelea kupitia kontenti kikamilifu.
Kwa hakika tuna furaha kukupa taarifa hii ya mageuzi na tunatumai kuwa itaboresha mafundisho yako.
Kama kawaida, majibu yako ni ya maana sana kwetu, hivyo basi kuwa huru kutupa fikira zako na mapendekezo yako.
Jiunge nasi kwa kujisajilisha kwenye jarida letu na kutufuatilia katika mitandao yetu ya kijamii.
Usikivu Mwema!
60 dakika
60 dakika
90 dakika
Shutdown Academy
90 dakika
Shutdown Academy
Zana hii ya mtandao huwasaidia wanaharakati kukusanya ushahidi wa kukatizwa kwa muun
This article showcases a case study from our course ‘Detecting Internet Shutdowns with IODA’.
Idhinishwa: Kutambulisha Vyeti vya AASA kwa Watetezi Uhuru Wa Mtandao
The Advocacy Assembly Internet Shutdown Academy (AASA inatoa vyeti kwa wanafunzi wa mtandaoni ambao walimaliza kozi kumi zote katika programu za Shutdown Academy!
Changamoto na fursa kwaajili ya mpango mkakati wa kupingana na uzimwaji wa mtandao
Kama sehemu ya uchechemuzi unaofanywa na hii kozi ilikusanya meza ya majadiliano kwenye mpango mkakati kupingana na uzimwaji wa mtandao. Kwenye majadiliano Wataalamu walioongelea uzoefu wa changamoto wa uzimwaji mahakamani Kitaifa na kikanda na Kushea mazoezi kwenye mkakati wa kisheria.
Uhakiki wa Shutdown Academy Ya Advocacy Assembly katika mwaka wa 2023
Katika mwaka wa 2023 Shutdown Academy ya Advocacy Assembly ilifanikiwa sana katika kuendeleza upiganaji wa haki za kidijitali na kupigania haki za uzimaji mtandao kote ulimwenguni. Tuna furaha kushea na nyinyi mafanikio makubwa na miradi tulifanikisha mwaka huo, na kuonyesha shughuli ambazo tumefanya kwa muda wa mwaka mmoja.
Kichwa cha habari: kozi za kuzuia kuzimwa kwa mtandao
Uchechemuzi unazuia uzimwaji wa mtandao na ukatazaji wa watu kutoa maoni yao mtabdaoni. Watu wakikosa upatikanaji wa mtandao wanapoteza haki muhimu na fursa mbalimbali zinazopatikana ulimwenguni. Watu kutoka sehemu mbalimbali duniani wanapigania haki ya upatikanaji wa mtandao ikiwemo Mawakili, Waandishi wa habari na watetezi wa Haki za kibinadamu wanaungana kupinga vikali vitisho dhidi ya uzimwaji wa mtandao.
Kutetetea Uhuru wa Mtandaoni: Mashirika Matatu Yanahusika
Uhuru wa mtandaoni umetishiwa kimataifa kutokana na kuzidi kuwepo na udhibiti, uzimaji mtandao na kufuatiliwa. Hatua hizo zimeathiri uwezo wa watu kupata taarifa, kujieleza, na kuwasiliana na wengine mtandaoni. Katika blogu hii, tutajadili kuhusiana na mashirika hayo matatu. Kila shirika husika lilitupa ufahamu wao waliojifunza kutokana na hisia zao kutokana na kozi mpya kwenye Shutdown Academy.