Kutetetea Uhuru wa Mtandaoni: Mashirika Matatu Yanahusika

Uhuru wa mtandaoni umetishiwa kimataifa kutokana na kuzidi kuwepo na udhibiti, uzimaji mtandao na kufuatiliwa. Hatua hizo zimeathiri uwezo wa watu kupata taarifa, kujieleza, na kuwasiliana na wengine mtandaoni. Kwa Bahati nzuri, kuna mashirika yanapigana dhidi ya  uzimaji mtandao na udhibiti.

Katika blogu hii, tutajadili kuhusiana na mashirika hayo matatu. Kila shirika husika lilitupa ufahamu wao waliojifunza kutokana na hisia zao kutokana na kozi mpya kwenye Shutdown Academy.

1. Radio Free Europe/Radio Liberty (RFE/RL)

Radio Free Europe/Radio Liberty (RFE/RL) ni shirika la habari ambalo huimarisha umuhimu wa demokrasia kwa kutupa habari sahihi, zisizodhibitiwa na mjadala wazi katika nchi ambazo uhuru wa kujieleza umetishiwa na porojo ni nyingi. RFE/RL uhudumu katika nchi 23 na kutumia lugha 27. Shirika hili uripoti ukweli bila kutishiwa na msukumo na kujaribu kukwepa udhibiti pahali pana udhibiti wa mtandao.

Katika kozi yetu ya “Mitigating internet censorshipPatrick Boehler, mkuu wa mipangilio ya kidijitali katika Radio Free Europe/Radio Liberty, alionya dhidi ya “ndoto za uwazi” ambazo hutokea wakati serikali zinafunga tovuti za kibinafsi.

“Wewe kama mtumiaji, unaona kwamba mtandao kote unapatikana, na unahisi kama unaona ukamilifu wa taarifa ambazo zinakufaa au ukamilifu wa taarifa unazohitaji. Na 4udhibiti unalengwa unaondoa wachapishaji binafsi kutoka mjadala huo na unahatarisha kuiharibu.” Anasema.

Boehler alisisitiza hitaji la kukuza uhusiano ulioimara na hadhira pia kuendelea kuelimisha jamii kuhusiana na zana na mbinu za kukwepa udhibiti.


 

“Tunachokifanya pia ni kuwaalika hadhira kutuuliza maswali. Hivyo iwapo wana maswali, wanaweza kuandikia katika jukwaa lolote linalopatikana. Na tunakagua maswali haya na kuyajibu – maswali mengi wanayoweza kuwa nayo.” alisema.

2. VE Inteligente

Kozi zetu za “Kupunguza Udhibiti wa Mtandaoni” na “Kupunguza Uzimaji Mtandao

Zinatolewa kwa ushirikiano na mradi wa VE sin Filtro wa Ve inteligente. VE inteligente ni shirika la Venezuela ambalo limekuwa likinakilisha na kupinga udhibiti wa mtandao tangu 2014, na kuanika mashambulio ya mtandaoni yanayofadhiliwa na serikali, upoteaji wa mtandao na pandashuka nyingine na kuboresha usalama wa kidijitali katika mfumo wazi. 

Mbali na kutayarisha kozi, Valentina Aguana na Andrés Azpúrua kutoka VE Inteligente walitoa hisia zao kuhusiana na uzimaji wa mda mrefu nchini Venezuela mnamo 2019 kama sehemu ya kesi ya kutafitiwa.

“Kitu cha kwanza ambacho tulijifunza ni daima kutarajia kisichotarajiwa na kibaya zaidi, ambacho ni ukosefu wa nguvu na kutokuwa na mtandao kwa wengi, kwa siku nyingi. Baada ya mapito hayo, tuko tayari na jamii yetu iko imara,” Aguana alisema.

Kwa kufuatilizia hali za kisiasa kujua uwezekano wa uzimaji kutayarisha zanakazi katika mawasiliano hata wakati wa ukatizwaji kabisa, timu ya VE inteligente ilisisitiza umuhimu wa kuimarisha utayarifu wa jamii.   

“Wape wanafamilia ujuzi ambao umepata, rafiki na jamii, kwa sababu vile umegundua, uimara wa suluhu hizi utegemea na uasilishaji mpana wa kijamii.” - Andrés Azpúrua, VE inteligente.

3. TunnelBear

TunnelBear ni huduma ya VPN ambayo inaruhusu watumiaji kukwepa udhibiti wa mtandao na kupata mtandao bila tatizo. Kampuni hii ya Canada kwa muda mrefu ilipigania uhuru wa mtandao kwa ushirikiano na mashirika washirika. Katika wakati mzozo na udhibiti TunnelBear ilijikakamua, kwa kutoa bandoo kwa matumizi, vile ilikuwa Venezuela na Ukraine.

Katika mahojiano kuhusu kozi “Kupunguza Udhibiti wa Mtandao” Dave Carollo, ambaye ni meneja wa bidhaa TunnelBear, alisisitiza hitaji la uangalifu wakati wa kuteua ni huduma gani ya kutumia ya VPN.

“Kukiwa na huduma ya VPN, unafaa siku zote kutathmini sera za ufaragha kwa sababu kitu cha maana unafaa kuangalia ni kuwa kama inachukua data zozote za kutumia na kuzifanyia chochote. Hauhitaji huduma ya VPN ambayo inachukua data zako za matumizi liwe liwalo,” anasema.

Kwa zaidi ya miaka sita iliyopita, TunnelBear ilitokea kuwa ya kwanza ya VPN ya kuchapisha mshirika-wa tatu kwa utathmini wa kiusalama kwa umma. Miradi hii wazi ni vigezo ambavyo unafaa kutilia maanani wakati unafanya uamuzi wa huduma ya VPN.

“Nitatafuta huduma ya VPN ambayo ina utathmini wa kiusalama ambao wafanyia huduma zao ambazo wanaweka majibu wazi kuhusu. Au utathmini wa wazi ni aina nyingine za utathmini ambao watoaji wa VPN wanaweza kufanya pale ambapo wanaweka wazi kuhusu maombi wanapokea kutoka kwa serikali kuhusiana na taarifa za watumiaji.” Dave Carollo meneja wa bidhaa TunnelBear.

Miradi pamoja na mashirika kama Initiatives and organisations like Ve inteligente, Radio Free Europe/Radio Liberty (RFE/RL), na TunnelBear wanaendelea kupigana dhidi ya uhuru na uwazi wa mtandaoni. Kwa kutoa taarifa sahihi, kukuza usalama wa kidijitali, na kutoa zana za kukwepa udhibiti, mashirika haya yanasaidia jamii kupata mtandao bila tatizo.

Visa vya utafiti ni miongoni mwa kozi mpya “Kupunguza Udhibiti wa Mtandao” na “Kupunguza Uzimaji Mtandao” kutoka katika Internet Shutdown Academy. Shule ina kozi 10 katika lugha saba, na kufundishwa na wataalam kutoka mashirika makubwa na inalenga kueleimisha wanaharakati, wanahabari, na yeyote ameathiriwa na uvurugaji mtandao na udhibiti wa mtandaoni.

Kozi zinazohusiana

  • 60 dakika

    Shutdown Academy

    Kichwa cha Kosi : Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao

    WITNESS

    60 dakika

    WITNESS
  • Open Observatory of Network Interference (OONI)

    90 dakika

    Open Observatory of Network Interference (OONI)

Blogu

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
  • Faragha
  • Maagizo