Kutuhusu

Advocacy Assembly

Advocacy Assembly ni jukwaa wazi la mafunzo-mtandaoni linalohusisha kozi mbalimbali za wanaharakati wa haki za binaadamu, wahamasishaji na wanahabari. Ilianzishwa mnamo mwaka wa 2015, Advocacy Assembly awali ilidhamiriwa kuwa nafasi ya kufundisha wanafunzi ambao walihudhuria hafla wao binafsi. Kozi zetu zinafanywa na watu kutoka nchi zaidi ya 175 kote ulimwenguni. Wanafunzi hupata cheti wanapomaliza kila kozi ya mtandaoni. Jukwaa letu huwapa watu nafasi ya kuimarisha uelewa na ujuzi wao ili kuleta mabadiliko. Tunatoa kozi zenye mada mbalimbali, ikiwamo utetezi, sheria ya haki za binaadamu, haki za kidijitali, sayansi ya data, usanifu, usalama wa kidijitali, uanahabari wa kupeleleza, podikasti, uzimaji mtandao na uchanganuzi wazi wa taarifa. Pamoja na mashirika zaidi ya 20 tunaoshirikiana, tunaendelea kuzindua kozi mpya kila mara katika lugha tofauti kila mwaka. Jiunge nasi kwa kujisajili kwenye jarida letu na kutufuata kwenye mitandao yetu ya kijamii.

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji

Tufuate katika mitandao ya kijamii

Pata kozi za hivi punde kwenye kabrasha.

Jiandikishe kupata jarida letu leo

0
0
  • Faragha
  • Maagizo