Elekezwa

Maswali Yanayoulizwa Kila Mara

Una swali jinsi ya kupitia tovuti yetu? Advocacy Assembly ipo hapa kukusaidia. Soma maswali yanayoulizwa kila mara ya hivi punde hapa chini. Haupati unachotafuta? Wasiliana nasi kupitia ukurasa wetu wa Wasiliana Nasi.

advocacy Assembly ni jukwaa la lugha nyingi la mafunzo-mtandaoni kwa wanaharakati wa haki za binaadamu, wahamasishaji na wanahabari. Yeyote anaweza kujiunga na Advocacy Assembly na kufaidi kozi zetu za mtandaoni za bure.

Kozi zetu zinamfaa mtu yeyote ambaye anataka kusoma kuhusiana na utetezi, uanahabari, haki za binaadamu, sayansi data, uslama wa kidijitali, uvurugaji wa mtandao, na udhibiti wa mtandao.

Pale Juu kabisa ya ukurasamsingi bofya Kozi ukifuata na Ukurara wa Kozi Zote. Unaweza chagua kozi kutegemea zile zimechapishwa karibuni na zile unapendelea. Tutakukumbusha kozi mpya katika jarida letu.

Walimu wetu ni bora na wataalamu kutoka baadhi ya mashirika bora zaidi ya haki za binaadamu, vilevile kutoka mashirika ya habari.

Kila kozi mtandaoni inasomeshwa bure na imejumuisha sura na masomo kadhaa. Masomo yaneweza kuwa slaidi, vidio au maswali. Pia tunatoa vifaa mwisho wa kila somo kwa kujifundisha zaidi, kurasa za maelekezo na maelezo mengine muhimu. Kwa kusomea kozi na kupata cheti unafaa kuchagua kozi na kuchagua kitufe cha kujisajili baada ya kuingia kwa kutumia jina lako na nywila. Kwa kupakua cheti baada ya kumaliza kila kozi, sharti umalize kozi yote ili ukipate mwishoni. Iwapo hujajiunga bado, fungua akaunti yako bure, thibitisha baruapepe yako, ingia na bofya kitufe cha kujisajili kwenye kozi unayopendelea. Tafadhali zingatia kuwa tu ni watumiaji wanaoingia kutumia baruapepe na nywila watapata vifaa vya kozi yote.

Kama ungependa kujiondoa kutoka jarida letu, bofya tu kiungo cha kujiondoa chini ya baruapepe ambayo umepokea. Unaweza pia kusasisha mipangilio ya vikumbusho vya baruapepe yako katika mpangilio wa akaunti yako.

Pindi umepata kozi unayotaka kusomea na umeingia, bofya kitufe cha kujisajili. Hivyo tu!

Advocacy Assembly jukwaa la mafunzo-mtandaoni lililo na lugha nyingi. Hii inamaanisha huwezi kukutana na mwalimu moja kwa moja. Kama unataka kuanza mjadala au kutupa maoni yako, tunakushauri uwasiliane nasi kupitia Ukurasa wetu wa Kuwasiliana Nasi.

  1. Make sure your password is correct. If you have forgotten your password, please reset your password.
  2. If you are sure the password is correct or you reset your password and still can not log in, try to use your email address instead of your username. 
  3. If you are using a VPN, make sure your connections over the VPN works. 
  4. If none of the above works, try a different browser. If you are using chrome, try it in incognito mode. 

Pata kozi za hivi punde kwenye kabrasha.

Jiandikishe kupata jarida letu leo

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
  • Faragha
  • Maagizo