Zana hii ya mtandao huwasaidia wanaharakati kukusanya ushahidi wa kukatizwa kwa muun

Mamlaka kandamizi zinaendelea kupelekea kuzimwa kwa mtandao na kukatizwa kwa mtandao ili kuzuia ufikiaji wa habari kwa watu walio ndani ya maeneo yaliyoathiriwa, kuwatenga na ulimwengu wa nje na hivyo kuzuia  na kukiuka haki za binadamu. 

Takwimu za mwaka uliopita zinaonyesha kuwa matukio ya kuzimwa kwa intaneti duniani kote yalifikia angalau visa 186 vilivyorekodiwa katika nchi 35, ni idadi kubwa zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha mwaka mmoja. 

Nchini Irani, mara 18 kuzimwa kwa intenetu kulirekodiwa mnamo mwaka 2022 pekee. Wengi walikuwa wakiandamana na wengine kutoa wito wa maandamano

Katika kozi yetu ya ‘Kuchunguza kuzimwa kwa mtandao kwa kutumia IODA’, Amir Rashid, mkurugenzi wa haki za kidigitali na usalama katika Miaan Group, alizungumza kuhusu jinsi watetezi wa haki za binadamu wanaweza kutumia zana ya IODA kutambua na kuripoti kuhusu kukatizwa kwa muunganisho wa mtandao. 

Inafanyaje kazi?

IODA hutoa dashibodi inayopatikana kwa umma ambayo inaonyesha kwa ukaribu data ya wakati  halisi kwenye muunganisho wa mtandao katika Nchi, eneo na kiwango cha muendeshaji wa mtandao. Hatua hizi hukusanywa katika muda halisi kwa ufatiliaji wa mara kwa mara wa mtandao. 

Jinsi ya kutumia 

Dashibodi ya IODA huruhusu watumiaji kutafuta nchi, eneo au mtoa huduma mahususi wa inteneti na kuchagua kipindi. Ina njia mbili tofauti za kuibua data ambazo ni iliyorahisishwa na ya juu.

IODA ni muhimu kwa jumuiya ya uhuru wa mtandao kwa sababu wanaweza kuona ushahidi, muda, na eneo la kukatika na kuzimwa kwa muda kwa karibu muda halisu. Mafunzo ya hatua kwa hatua yanapatikana katika kozi yetu ya kugundua kuzima kwa mtandao IODA’.

Jinsi ya kuchunguza muktadha wa ndani?

Kuzimwa kwa mtandao nchini Irani hutokea katika viwango mbalimbali, kutoka kwa usumbufu wa ndani hadi kukatika kwa nchi nzima. Serikalo inaweza kudhibiti ufikiaji wa mtandao kwa kuchagua kupitia mtandao wa kitaifa wa habari (NIN), unaojulikana pia kama internet ya Irani. Jambo muhimu ni kwamba mtindo huu wa kuzima ulitoa kiwango cha kisasa zaidi cha ufikiaji wa viwango vinavyoruhusu mamlaka kukataa kuzima. 

Tovuti ya IODA inatupa taswira pana ya nchi ili kuelewa vyema kinachoendelea.”

Amir Rashidi, Director of Digital Rights & Security at the Miaan Group

Amir Rashid, Mkurugenzi wa Haki za kidigitali na usalama katika kikundi cha Miaan 

FilterWatch inategemea zana kama vile IODA kufuatilia kuzima kwa mtandao, kupata maarifa kuhusu matukio kama vile maandamano yanayokuja. Kwa kutambua usumbufu unaoweza kujitokeza wanaweza kuandika matukio haya na kuwapa wanaharakati ndani ya Iran zana muhimu za kupinga upotoshaji wa mamlaka na kutetea haki za kiraia. 

Hii inawapa wanaharakati uthibitisho thabiti wa kukatika kwa muunganisho. 

“Kujitayarisha kwa zana zinazotoa data ni muhimu sana ili kutoa changamoto kwa mamlaka kuhusu taarifa potofu wanazotoa hasa ndani ya nchi”

Amir Rashidi, Mkurugenzi wa Haki za Kidigitali na Usalama katika kikundi cha Miaan.

Huu ni uchunguzi kifani kutoka kwenye kozi yetu ya ‘Kuchunguza Kuzimwa kwa Mtandso kwa kutumia IODA’, Katika chuo chetu cha kuzimwa kwa mtandao, ambacho huangazia kozi 10 katika lugha saba, zinazofundishwa na wataalamu kutoka mashirika mashuhuri. Imeundwa kuelimisha wanaharakati, wanahabari,  na mtu yeyote aliyeathiriwa na kukatizwa kwa mtandao na uthibiti wa mtandaoni. 

Kozi zinazohusiana

 • 60 dakika

  Shutdown Academy

  Kichwa cha Kosi : Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao

  WITNESS

  60 dakika

  WITNESS
 • Open Observatory of Network Interference (OONI)

  90 dakika

  Open Observatory of Network Interference (OONI)

Blogu

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
 • Faragha
 • Maagizo