Kichwa cha habari: kozi za kuzuia kuzimwa kwa mtandao

Sio siri tena…Uchechemuzi unazuia uzimwaji wa mtandao  na ukatazaji wa watu kutoa maoni yao mtabdaoni. Watu wakikosa upatikanaji wa mtandao wanapoteza haki muhimu na fursa mbalimbali zinazopatikana ulimwenguni.  Watu kutoka sehemu mbalimbali duniani wanapigania haki ya upatikanaji wa mtandao ikiwemo Mawakili, Waandishi wa habari na watetezi wa Haki za kibinadamu wanaungana kupinga vikali vitisho dhidi ya uzimwaji wa mtandao.

Hii ndo sababu kubwa ya kuanzisha kozi hii. Ili kutoa uzoefu.  Ili kujifunza matumizi ya vifaa katika kampeni za kupinga uzimwaji wa mtandao. Kuhakikisha kupata uelewa na kufanya maamuzi.

Hizi kozi kumi ni bure na binafsi. Zimetengenezwa kwa kushirikiana na wataalamu kutoka mashirika yanayojulikana  kwa kufanya kazi na  mashirika kama Access Now, OONI, WITNESS, The Intenert  Intelligence Lab (IODA) , The Global Network Intiative (GNI), Internews, Ve Intelligente na Center for Law na Democracy. Katika kila kozi utasikiliza uzoefu wa Waandishi wa habari , Mawakili , Wataalamu wa haki na sheria ba Makundi ya kijamii.

 Unatamani kujua zaidi? Tunakupitisha katika mambo muhimu yalioanishwa katika kila kozi.

1. Utangulizi katika uzimwaji wa mtandao (Access Now)
Hii kozi  inatambulisha mambo muhimu ya kuzingatia katika uzimwaji wa mtandao, athari zake  kwa haki za binadamu na njia gani Mamlaka zinazima mtandao  katika siku zilizopita. Utaona namna ambavyo upiganaji wa kidunia dhidi ya uzimwaji wa mtandao ikiwemo #KeepItOn coalition inatumia watu mbalimbali kufanya uchechemuzi wa kumaliza uzimwaji wa mtandao.

2. Kugundua uzimwaji wa mtandao kwa kutunia IODA (IODA)
Je unafanya tafiti ya mtandao kuzima? Je Mamlaka zinapinga uwepo wake ? Unataka kupata uthibitisho? Kuona zaidi. Kwenye kozi hii utajifunza IODA, kupima uwepo wa mtandao na namna unavyofanya kazi. Pia utajifunza matumizi yake katika kuangalia uzimwaji wa mtandao uliopo na uliopita.

3. Kupima uzimwaji wa mtandao kwa kutumia kifaa cha OONI na data za wazi
Vipi kama unaweza kufuatilia ukosekaji wa mtandao duniani na kuwatia hatiani wenye Mamlaka ? Hiki ndicho utakachojifunza katika kozi hii. Utapata nafasi ya kupita hatua kwa hatua namna ya kupima uzimwaji wa mtandao. Pia utajifunza kugundua taarifa zinazozuiwa duniani kwasababu hakuna tena uhalifu unaofichika.

4. Kuweka kumbukumbu za ukiukwaji wa Haki za Kibinadamu wakati wa Uzimwaji mtandao
Mamlaka zinapoleta amri ya uzimwaji wa mtandao wanazuia kupata taarifa za ukiukwaji wa haki za binadamu . Kwenye kozi hii utajifunza kupata taarifa kwa usalama hata katika kipindi ambacho mtandao haupatikani. Hii kozi  ni ya vitendo na inatoa ushauri kwa mashirika yanayotetea haki za binadamu lakini hayana uwezo mkubwa.

5. Kupunguza kuzimwa kwa mtandao
Kwenye kozi hii utajifunza namna uzimwaji wa mtandao unavyofanya kazi na kuelewa kwa kina . Kugundua namna ya kujilinda wewe na wenzio katika kipindi kigumu  na kupunguza madhara.

6. Kupunguza  udhibiti wa ukosefu wa mtandao 
Kama unapata shida kupata vifaa vya kuwa mtandaoni jiunge na kozi hii ni chaguo sahihi kwa muda huu.

7. Kuanzisha mpango maalumu wa uzimwaji mtandao
Kama umechoka kukosa mtandao na uko tayari kumaliza hali hii. Hii kozi itakufundisha namna ya kuelewa na kufanya uchechemuzi kwaajili ya changamoto zilizopo katika jamii ili kuzuia uzimwaji wa mtandao. Hii kozi inatoa utaratibu kwa vitendo ili mtu aweze kujijenga na kujiandaa kwaajili ya kujilinda na kupinga vitendo vya uziimwaji wa mtandao.

8. Kushirikiana na Sekta binafsi kumaliza tatizo la uzimwaji wa mtandao
Ushawahi kujiuliza je mashirika na biashara zinasimama upande gani likija suala la uzimwaji wa mtandao? Maana kazi nyingi zinategemea mtandao sikuhizi. Watoaji huduma za ktandao anaweza kuwa sekta binafsi . Hii kozi itajibu maswali hayo. Pia utajifunza namna ya kushirikiana na sekta binafsi na kufanya kampeni za kuzuia uzimwaji wa mtandao. Cha nyongeza ni kuwa utagundua namna mashirika yanapokea amri za kuzima mtandao.

9. Kutumia shauri la mkakati kumaliza uzimwaji wa mtandao (CLD)
Uzimwaji wa mtandao ni haki kisheria ? Je unaweza ukaenda mahakamani na kujaribu kumshtaki mtu anayehusika. Hapa linakuja wazo la kuwa na mpango mkakati wa kushughulika na uzimwaji wa mtandao. Hii kozi itakuelewesha haki ya kisheria za kufuata na namna ya kujitetea  mahakamani katika kumtuhumu atakayehusika na uzimwaji wa mtandao.

10. Uchechemuzi na Kampeni za kupinga Uzimwaji wa mtandao
Unaweza ukawa ushaona uchechemuzi na  nguvu ya jamii katika kupinga uzimwaji wa mtandao. Katika kozi hii tutagundua makundi mbalimbali yanayosababisha uzimwaji wa mtandao na kupitia mifano halisi tutajifunza namna Watu huko Duniani wanavyopingana na uzimwaji wa mtandao.

Kozi kumi, kugha saba na zaidi ya mifano halisi ishirini inapatikana kwaajili yako. Kila kozi inachukua takribani dakika 60 mpaka 90 kukamilisha. Anza sasa kujifunza kwa manufaa yako bila kulipia chochote.

Jiunge sasa!

Kozi zinazohusiana

 • 60 dakika

  Shutdown Academy

  Kichwa cha Kosi : Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao

  WITNESS

  60 dakika

  WITNESS
 • Open Observatory of Network Interference (OONI)

  90 dakika

  Open Observatory of Network Interference (OONI)

Blogu

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
 • Faragha
 • Maagizo