Uzimaji wa Mitandao unaendelea duniani, na kuwaacha mamilioni ya watu kwa hali tete. Lakini nini athari ya uvurugaji wa mtandao? Tuliuliza mamia ya wanaharakati, wanafunzi, wanahabari, wakulima na wafanyabiashara kuhusu maoni yao ikiwa kama sehemu ya Mradi wa Mafundisho ya Ukuzaji ya Advocacy Assembly. Walielezea mtiririko wa madhara, huku uzimaji ukisababisha kutofikia taarifa, kutopata huduma za dharura na kutopata uchumi bora.
“Niliishi kama zamani,” akasimulia wakili na mshiriki wa mradi wa mafundisho ya AA-ISA kutoka Cameroon. Kwa miezi mitatu, serikali ilikata mtandao katika maeneo ya raia wanaozungumza Kiingereza nchini humo. Mshiriki huyo alielezea jinsi alilazimika kusafiri hadi mji ulio karibu ili kuangalia baruameme yake. Huduma yake ya sheria haikuweza kufikia waathiriwa husika.
Many of the participants told us how shutdowns invade almost every facet of life - education, health, family, and work. A student from Tanzania described her anguish when universities abruptly shifted Stori yake si tofauti. Kama sehemu mojawapo wa kuitisha maombi ya Mradi wa Mafundisho ya Ukuzaji ya Advocacy Assembly, tulipokea maombi zaidi ya 1,060 kutoka nchi 135 kushiriki katika mradi wa wiki-saba ambao ulianza Septemba hadi Novemba 2023. Stori washiriki walituambia kuhusiana na hali ya ukatishwaji mtandao inaangazia madhara makubwa yanayosababishwa kwa ukatishwaji huo na serikali- na kuonyesha kuwa kuna haja ya kuweka msingi imara kwa watu ulimwenguni ili kujiandaa na kupigana dhidi ya uzimaji.
Washiriki wengi walituambia jinsi uzimaji huo unaathiri kila kona ya maisha – elimu, afya, familia na kazi. Mwanafunzi kutoka Tanzania alielezea machungu yake wakati vyuo vikuu vilihamisha masomo kuenda mtandaoni wakati wa COVID-19. “Uvurugaji wa ghafla mtandaoni uliathiri kushiriki kwangu kikamilifu masomo yangu ya mtandaoni na kutokamilisha kazi zangu,” aliandika. Gredi zangu zilishuka. Mustakabali wake haujulikani. Kwa mama ya mwanafunzi huyu, ukatishwaji huu ulipunguza riziki na ajira. Biashara yake ya mtandaoni iliathirika, na kuweka familia katika hali ngumu ya kifedha. Mshiriki mwengine, mwanabiashara wa kilimo kutoka nchini Nigeria, alieleza jinsi anatumia “mtandao kutangaza bidhaa zake za shambani.” Wakati mtandao ulizimwa, aliripoti kuwa “mauzo yetu yalipungua sana."
Kwa wanaharakati walio mstari wa mbele katika chaguzi kuu au migogoro ya kisiasa, uzimwaji ulimaanisha kukosa haki ya kujumuika wakati shughuli zimeshika kasi. Mfuatiliaji wa uchaguzi nchini Tanzania alishindwa kutuma ripoti za udanganyifu. Mtetezi wa haki za binadamu alituambia alikuwa ananakili visa vya dhuluma katika eneo la Oromia la Ethiopia na kuwa uzimaji mwingi “ulisababisha ugumu kwangu na mwenzangu kufikia waathiria”. Nchini Zimbabwe, mwanahabari alituelezea kuwa alikuwa anafanya stori ya maandamano ambayo ilikuwa imepangwa na upinzani ambao yalikuwa na ghasia. Aliandika, “serikali ilizima mtandao na hakuna aliyejua kilichokuwa kikiendelea nchini Zimbabwe… bila kujua nani alikuwa amekufa.” Nchini India, mshiriki alieleza jinsi ufungaji majukwaa ya kijamii kama WhatsApp eneo la Manipur ilisababisha fujo kwa kuenezwa habari za urongo.
Hofu na hali ya wasiwasi iliwajaa wengi kwa sababu hatukuwa na taarifa sahihi au kuipata mapema,” alikumbuka mshiriki mmoja kutoka Uganda. Alisema kuwa kwa siku saba, yeye na zaidi waganda milioni 45 waliwekwa gizani na kutenganishwa na wapendwa wao na taarifa.
Licha ya stori hizi za kugandamiza na kutenga athari za uzimaji mtandao, wengi wa washiriki walikuwa na matumaini kuhusiana na juhudi zao za kupigana na ari ya kujifunza na kuunganishwa na wanaharakati wengine. Baadhi ya washiriki walielezea jinsi walijifunza kutumia zana ya upimaji kama OONI kunakili matukio ya uzimaji mtandao, na ni vipi hii imewawezesha kutumia ushahidi huu ili kuwajibisha serikali. Mshiriki mmoja alieleza vile kundi la mawakili kutoka Senegal ambao wamekuwa wakishirikiana ili kuelewa athari za uzimaji kisheria. Mshiriki mwengine aliandika kuhusiana na uwepo wa shirikisho la wanaharakati wa haki za kimitandao wanaopigana dhidi ya uzimaji katika mipaka nchi, akisema “ nataka kampeni yangu isiwe tu na matokeo katika jamii yangu kwa uhamasishaji na uimarishaji lakini pia kujifunza kutoka kwa matokeo na kushea huduma bora na wenzio kutoka nchi nyingine.” Mshiriki mwengine kutoka Nigeria alielezea jinsi jamii yake “watu huona uvurugaji mtandao kama hali ya kawaida na kitu cha kutarajiwa.” Aliandika kuwa alikuwa anataka kushiriki katika mafundisho “kuwaonyesha kuwa hii si kawaida na sharti tuwajibishe serikali na wafuasi wao wakati kutokea uzimaji mtandao.”
Kwa sababu ya maombi mengi ya kutaka kuwa na Mradi wa Mafunzo ya Ukuzaji wa AA-ISA wa kwanza, tumeamua kuendesha huu mradi kuanzia Februari hadi Aprili 2024. Mradi huu utakufaa na kukupa maelekezo ya kijamii huku ukisomea kozi kumi za Advocacy Assembly Internet Shutdown Academy, na pia nafasi za kukutana na wakuzaji, wataalam na wafadhili. Utajifunza ujuzi mwingi unaohusiana na uhamasishaji dhidi ya uzimaji mtandao upimaji wa kuzimwa mtandao, kutengeneza mchakato imara dhidi ya uzimaji mtandao, kushirikiana na sekta za kibinafsi, kunakili matukio ya ukiukaji haki wakati wa kuzimwa mtandao na kutumia utaratibu wa kisheria kushtaki.
Wanaharakati walio na uzoevu pamoja na wale wapya kwa masuala ya uhuru wa mtandao wanahimizwa kutuma maombi. Pamoja, tunawezesha ushirikiano ili #KeepItOn dhidi ya udhibiti na uzimaji.
Jifunze zaidi kuhusiana na mradi huo na tuma maombi kwa kundi litakalochukuliwa na Akademi kwa kubofya kiungo hiki.
60 dakika
60 dakika
90 dakika
Shutdown Academy
90 dakika
Shutdown Academy
Zana hii ya mtandao huwasaidia wanaharakati kukusanya ushahidi wa kukatizwa kwa muun
This article showcases a case study from our course ‘Detecting Internet Shutdowns with IODA’.
Idhinishwa: Kutambulisha Vyeti vya AASA kwa Watetezi Uhuru Wa Mtandao
The Advocacy Assembly Internet Shutdown Academy (AASA inatoa vyeti kwa wanafunzi wa mtandaoni ambao walimaliza kozi kumi zote katika programu za Shutdown Academy!
Changamoto na fursa kwaajili ya mpango mkakati wa kupingana na uzimwaji wa mtandao
Kama sehemu ya uchechemuzi unaofanywa na hii kozi ilikusanya meza ya majadiliano kwenye mpango mkakati kupingana na uzimwaji wa mtandao. Kwenye majadiliano Wataalamu walioongelea uzoefu wa changamoto wa uzimwaji mahakamani Kitaifa na kikanda na Kushea mazoezi kwenye mkakati wa kisheria.
Uhakiki wa Shutdown Academy Ya Advocacy Assembly katika mwaka wa 2023
Katika mwaka wa 2023 Shutdown Academy ya Advocacy Assembly ilifanikiwa sana katika kuendeleza upiganaji wa haki za kidijitali na kupigania haki za uzimaji mtandao kote ulimwenguni. Tuna furaha kushea na nyinyi mafanikio makubwa na miradi tulifanikisha mwaka huo, na kuonyesha shughuli ambazo tumefanya kwa muda wa mwaka mmoja.
Kichwa cha habari: kozi za kuzuia kuzimwa kwa mtandao
Uchechemuzi unazuia uzimwaji wa mtandao na ukatazaji wa watu kutoa maoni yao mtabdaoni. Watu wakikosa upatikanaji wa mtandao wanapoteza haki muhimu na fursa mbalimbali zinazopatikana ulimwenguni. Watu kutoka sehemu mbalimbali duniani wanapigania haki ya upatikanaji wa mtandao ikiwemo Mawakili, Waandishi wa habari na watetezi wa Haki za kibinadamu wanaungana kupinga vikali vitisho dhidi ya uzimwaji wa mtandao.
Kutetetea Uhuru wa Mtandaoni: Mashirika Matatu Yanahusika
Uhuru wa mtandaoni umetishiwa kimataifa kutokana na kuzidi kuwepo na udhibiti, uzimaji mtandao na kufuatiliwa. Hatua hizo zimeathiri uwezo wa watu kupata taarifa, kujieleza, na kuwasiliana na wengine mtandaoni. Katika blogu hii, tutajadili kuhusiana na mashirika hayo matatu. Kila shirika husika lilitupa ufahamu wao waliojifunza kutokana na hisia zao kutokana na kozi mpya kwenye Shutdown Academy.