The Advocacy Assembly Internet Shutdown Academy (AASA inatoa vyeti kwa wanafunzi wa mtandaoni ambao walimaliza kozi kumi zote katika programu za Shutdown Academy!
Kuanzia leo, mwanafunzi yeyote anayejikakamua na kumaliza kozi zote kumi za Shutdown Academy anaweza kuomba cheti binafsi cha AASA, kutambulika rasmi kwa kuwa na ujuzi kamili kuhusiana na mada ya uzimaji mtandao. Cheti hiki si tu kinatambua kujitolea kwako kuelewa uvurugaji mtandao lakini pia inaashiria utayarifu wako wa kupigania haki za kidijitali.
Aprogramu ya AASA , iliindwa kwa kuwatia nguvu wanahrakati, wanahabari, na watu wanaoathiriwa na uzimaji mtandao na udhibiti, ina kozi katika lugha saba, na kufunzwa na wataalamu kutoka mashirika makubwa. Lengo letu ni kukufanya uelewe changamoto zinasababishwa na kuzimwa mtandao na kuwapa wanafunzi zana za kutumia na kupinga uvurugaji huo.
Kwa mtazamo wa kiteknikali wa uzimaji wa mtandao hadi mifumo ya kisheria na na mipango ya utetezi ya kuwa nayo, Shutdown Academy inaangazia mada kadhaa. Kwa kujipatia cheti cha AASA, unaonyesha ujuzi wa somo hili muhimu na kujiunga na jumuia ya watetezi kutetea haki za kidijitali.
Ili kupata cheti cha Shutdown Academy cha kukubalisha ujuzi wako wa kupinga uzimaji mtandao, fuata hatua hizi:
1- Maliza Kozi Kumi Zote za AASA:
Hakikisha kwamba umemaliza kozi zote kumi za programu za AASA, ili kuonyesha uelewa wako kuhusiana na changamoto zinazosababishwa ba uzimaji wa mtandao.
2- Tuma ombi lako:
Tuma baruapepe <[email protected]> ilioyo na mada: "Ombi la Cheti Cha AASA"
Katika baruapepe yako, toa maelezo yafutayo:
Majina yako kamili, jina unalotumia au baruapepe uliyotumia kufanya kozi.
3- Tupe jina la kwanza na jina la mwisho ambalo unapendelea liwe katika cheti chako:
Pindi tu ujumbe wako umeidhinishwa, utapokea cheti chako maalum cha AASA, ishara tosha kwa kujitolea kwako jinsi kupigana na uzimaji wa mtandao.
Jiandikishe sasa, kamilisha programu ya Shutdown Academy, na pata cheti chako!
Kitu kingine: iwapo ni sawa, usisite kusherehekea mafanikio yako na shea cheti chako cha AASA mtandaoni! Usisahau kututagi katika mitandao ya kijamii
60 dakika
60 dakika
90 dakika
Shutdown Academy
90 dakika
Shutdown Academy
Zana hii ya mtandao huwasaidia wanaharakati kukusanya ushahidi wa kukatizwa kwa muun
This article showcases a case study from our course ‘Detecting Internet Shutdowns with IODA’.
Changamoto na fursa kwaajili ya mpango mkakati wa kupingana na uzimwaji wa mtandao
Kama sehemu ya uchechemuzi unaofanywa na hii kozi ilikusanya meza ya majadiliano kwenye mpango mkakati kupingana na uzimwaji wa mtandao. Kwenye majadiliano Wataalamu walioongelea uzoefu wa changamoto wa uzimwaji mahakamani Kitaifa na kikanda na Kushea mazoezi kwenye mkakati wa kisheria.
Uhakiki wa Shutdown Academy Ya Advocacy Assembly katika mwaka wa 2023
Katika mwaka wa 2023 Shutdown Academy ya Advocacy Assembly ilifanikiwa sana katika kuendeleza upiganaji wa haki za kidijitali na kupigania haki za uzimaji mtandao kote ulimwenguni. Tuna furaha kushea na nyinyi mafanikio makubwa na miradi tulifanikisha mwaka huo, na kuonyesha shughuli ambazo tumefanya kwa muda wa mwaka mmoja.
Kichwa cha habari: kozi za kuzuia kuzimwa kwa mtandao
Uchechemuzi unazuia uzimwaji wa mtandao na ukatazaji wa watu kutoa maoni yao mtabdaoni. Watu wakikosa upatikanaji wa mtandao wanapoteza haki muhimu na fursa mbalimbali zinazopatikana ulimwenguni. Watu kutoka sehemu mbalimbali duniani wanapigania haki ya upatikanaji wa mtandao ikiwemo Mawakili, Waandishi wa habari na watetezi wa Haki za kibinadamu wanaungana kupinga vikali vitisho dhidi ya uzimwaji wa mtandao.
Kutetetea Uhuru wa Mtandaoni: Mashirika Matatu Yanahusika
Uhuru wa mtandaoni umetishiwa kimataifa kutokana na kuzidi kuwepo na udhibiti, uzimaji mtandao na kufuatiliwa. Hatua hizo zimeathiri uwezo wa watu kupata taarifa, kujieleza, na kuwasiliana na wengine mtandaoni. Katika blogu hii, tutajadili kuhusiana na mashirika hayo matatu. Kila shirika husika lilitupa ufahamu wao waliojifunza kutokana na hisia zao kutokana na kozi mpya kwenye Shutdown Academy.
Stori Ukakamavu kutoka Mradi wa Mafundisho ya Advocacy Assembly
Kwa sababu ya maombi mengi ya kutaka kuwa na Mradi wa Mafunzo ya Ukuzaji wa AA-ISA wa kwanza, tumeamua kuendesha huu mradi kuanzia Februari hadi Aprili 2024. Mradi huu utakufaa na kukupa maelekezo ya kijamii huku ukisomea kozi kumi za Advocacy Assembly Internet Shutdown Academy, na pia nafasi za kukutana na wakuzaji, wataalam na wafadhili.