Shutdown Academy

60 dakika

Kupunguza Udhibiti wa Mtandaoni

Ve Sin Filtro
Muhtasari:
Kozi hii itakusaidia kuelewa aina mbalimbali za udhibiti mtandao, ni vipi na ni muda upi utatokea na mbinu salama za kuzikwepa.
Kuhusu kozi hii:
Huku serikali dhalimu ikikazana kudhibiti uwepo na upataji wa taarifa, uwepo wa mtandao kila mahali kama jukwaa la uhuru wa kuzungumza inaifanya kuwa mlengwa mkuu kwa kudhibitiwa. Nchi kama China imeidhinisha udhibiti kama huo kupitia miundo-msingi ya uangalizi kama Great Firewall, kwa kuangalia na kudhibiti kile watu wanafanya mtandaoni, ambao ni ukiukaji wa haki za kibinaadamu. Katika kozi hii tutajifunza zaidi kuhusu udhibiti wa mtandao, tukitumia visa vingi vilivyotafitiwa kama mfano tukionyesha namna ya kutumia mbinu na zana za kukwepa kuzuiwa huku.
Najifunza nini:
Baada ya kozi, utaweza: ● Kuelewa udhibiti mtandao, unafanywa vipi, na unatokea lini ● Kuwa na mwongozo wa aina za udhibiti wa awali ukitumia visa vya vivyotafitiwa vya kutumiwa kama mfano ● Pitia aina za udhibiti ukitumia zana na mbinu zilizoteuliwa
Ni nini nafaa kujua:
Kozi hii imeundwa kwa ajili ya watu wanaoishi, kufanya kazi au kutoa uhuru wa mtandao na kusaidia usalama wa kidijitali kwa jamii katika maeneo yenye udhalimu.

Walimu

Andrés Azpúrua

Mkurugenzi Mkuu katika VE Inteligente. Mwanaharakati na pia mtafiti katika masuala ya usalama wa kidijitali, uanateknolojia wa kiraia na haki za kibinadamu mtandaoni. Andrés na kundi lake hutetea haki za mtandaoni za raia wa Venezuela na kusaidia kukinga wanaharakati na vyombo binafsi vya habari binafsi na Mashirika ya Kijamii.

Valentina Aguana

Valentina Aguana ni mwanaharakati wa haki za kidijitali kutoka Venezuela, ni mwanataaluma wa uhandisi wa kompyuta na mwanachama wa NGO VE Sin Filtro tangu 2019. Anafuatilia matukio ya udhibiti na huchanganua mashambulio ya mitandaoni ambayo yanalenga waasi kutoka serikali ya Venezuela. Valentina pia hufundisha wanahabari na wanaharakati kuhusiana na faragha na maswala ya usalama.

1.1 Kutana na mwalimu wenu & kuhusu kozi
1.2 Nini udhibiti wa mtandao?
1.3 Ni ipi tofauti baina ya udhibiti wa mtandao na uzimaji mtandao?
1.4 Ni vipi nitajua kuwa mtandao umedhibitiwa?
2.1 Ni vipi mtandao hufanya kazi
2.2 Uzuiaji Ruta na IP
2.3 Kuelewa jinsi ya kontenti zinafungwa
2.4 Kuelewa Ubanaji
2.5 Hata hivyo nini DNS
2.6 Wakati handisheki inafeli – TCP Ujifunga
2.7 Utumizi wa-kipengee kwa udhibiti/DPI
3.1 Kubadili mipangilio yako ya DNS / DoH / DNS kupitia TLS
3.2 Kukwepa vizuizi na VPN
3.3 Go bila mipaka na Tor
3.4 Kwenye Go na TAILS
3.5 CENO browser
4.1 Tovuti yako kuzuiwa: Hatua za kwanza na mambo ya kuzingatia
4.2 Kisa cha utafiti – VPN & Udhibiti wa mtandao
4.3 Kisa cha utafiti–Ni Radio Free Europe / Radio Liberty inavyokwepa udhibiti wa mtandao
4.4 Huduma zinazostahimili udhibiti na tovuti za mirrors
4.5 Ufiche wa Tovuti: HTTPS, ESNE na zaidi
5.1 Vidio ya kumalizia
5.2 Uchunguzi wa kozi

Kozi zinazohusiana

  • 60 dakika

    Shutdown Academy

    Kichwa cha Kosi : Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao

    WITNESS

    60 dakika

    WITNESS
  • Open Observatory of Network Interference (OONI)

    90 dakika

    Open Observatory of Network Interference (OONI)

usomaji unaopendekezwa

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
  • Faragha
  • Maagizo