Shutdown Academy

60 dakika

Kupunguza Uzimaji Mtandao

Ve Sin Filtro
Muhtasari:
Kozi hii itaonyesha baadhi ya mbinu ambazo zinaweza kupunguza baadhi ya athari zinazosababishwa na uzimaji mtandao katika jamii au shirika lako. Itaangazia kukuelewesha ni nini uzimaji Mtandao katika viwango vya kiufundi na ni vipi utajikinga pamoja na wengine wakati inatokea.
Kuhusu kozi hii:
Kozi hii imegawanyika kwa viwango vya sura, na kila moja imejumuisha mseto wa masomo ya vidio na maandishi yaliyoundwa hususan kwa kila mada. Kozi hii pia ina mafunzo kutoka maeneo ambayo yameathirika kutokana na uzimwaji mtandao siku za awali.
Najifunza nini:
Tambua tofauti baina ya dhana kama vile “uzimaji mtandao” na “ukatizaji mtandao”, na mbinu kadhaa za kuwasiliana kupitia aina tofauti za uzimaji na ukatizaji mtandao.
Ni nini nafaa kujua:
Uelewa wa kimsingi wa uzimaji mtandao na ni vipi unatathmini hatari ya uzimaji uliopo. Kozi uendeleza uelewaji wa jumla wa viunzi vya utumaji jumbe za mtandaoni, kutumia broasa za mtandao, na jinsi ya kusakinisha na kupakua viunzi.

Walimu

Andrés Azpúrua

Mkurugenzi Mkuu katika VE Inteligente. Mwanaharakati na pia mtafiti katika masuala ya usalama wa kidijitali, uanateknolojia wa kiraia na haki za kibinadamu mtandaoni. Andrés na kundi lake hutetea haki za mtandaoni za raia wa Venezuela na kusaidia kukinga wanaharakati na vyombo binafsi vya habari binafsi na Mashirika ya Kijamii.

Valentina Aguana

Valentina Aguana ni mwanaharakati wa haki za kidijitali kutoka Venezuela, ni mwanataaluma wa uhandisi wa kompyuta na mwanachama wa NGO VE Sin Filtro tangu 2019. Anafuatilia matukio ya udhibiti na huchanganua mashambulio ya mitandaoni ambayo yanalenga waasi kutoka serikali ya Venezuela. Valentina pia hufundisha wanahabari na wanaharakati kuhusiana na faragha na maswala ya usalama.

1.1 Utangulizi wa kozi
1.2 Uzimaji Mtandao: Maelezo mafupi & na mbinu ibuka
1.3 Aina ya Uzimaji Mitandao na masharti husika
1.4 Kuangalia uwezekano: Kufuatilia visa vya kisiasa & matarajio
2.1 Ni vipi unakisia uwepo wa uzimaji?
2.2 Athari za uzimaji mtandao ni zipi?
2.3 Jitayarishe dhidi ya uzimaji mtandao vile unajitayarisha dhidi ya majanga asili
2.4 Kisa cha utafiti – Uzimaji mtandao nchini Venezuela
2.5 Kutambua na kuimarisha mifumo dhaifu katika uzimaji mtandao
3.1 Ukwepaji na Bila Kujulikana wakati wa Uzimaji
3.2 VPN ni nini?
3.3 Kufikia mtandao na VPN
3.4 Kisa cha utafiti – Kukwepa uzimaji mtandao nchini Kazakhstan
3.5 Quiz - VPNs
4.1 Mbinu na mikakati ya nje ya mtandao ya mawasiliano salama
4.2 Utumaji Jumbe na Kiunzi cha Silence – Tumia Mattukio na Vikwazo
4.3 Kutumia kiunzi cha Briar wakati wa ukosefu wa mtandao
4.4 Huduma za nyumbani na Delta Chat – hutumia matukio & vikwazo
4.5 Kutumia njia za zamani na bila mtandao
5.1 Hitimisho
5.2 Uchunguzi wa kozi

Kozi zinazohusiana

  • 60 dakika

    Shutdown Academy

    Kichwa cha Kosi : Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao

    WITNESS

    60 dakika

    WITNESS
  • Open Observatory of Network Interference (OONI)

    90 dakika

    Open Observatory of Network Interference (OONI)

usomaji unaopendekezwa

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
  • Faragha
  • Maagizo