Shutdown Academy

120 dakika

Kutumia Mkondo wa mashtaka Kupigana na Uzimaji Mtandao

Centre for Law and Democracy
Muhtasari:
Kozi hii inaangazia jinsi ya kutumia mkondo wa mashtaka kupinga ulazimishaji wa uzimaji mtandao na kutafuta fidia dhidi ya uvurugaji unakotokea. Kimsingi umeundwa kuwafaa watetezi na mawakili ambao wanalenga kupanua kazi yao ya utetezi kwa kutumia mkondo wa mashtaka.
Kuhusu kozi hii:
Uzimaji mtandao, iwe kitaifa au baadhi ya maeneo ya taifa na iwapo ni moja kwa moja au kwa polepole, umeenea sana kwa muda wa miaka kati ya 10-15. Kuna njia kadhaa za kukabiliana na hatua hii ya serikali, ambapo mojawapo ambayo imefaulu pakubwa katika mataifa kadhaa ni utumiaji wa mkondo wa mashtaka. Hii inaweza kuharamisha uzimaji unaoendelea, imeweka viwango ambapo hakutakuwa na uwezekano wa uzimaji, au kuna uwezekano wa fidia kwa hasara iliyosababishwa na uzimaji. Mkondo wa mashtaka si rahisi kutekeleza lakini, kuzingatia hali ya athari za uzimaji mtandao, ni muhimu kuuzingatia miongoni mwa mbinu nyingine.
Najifunza nini:
Kozi hii inaangazia viwango vya uwajibikaji vya Mataifa kuhusiana na haki za kibinadamu katika kuheshimu uhuru wa kujieleza, kwa kumlika zile zinazohusiana na uzimaji Mtandao. Baadaye inatoa utathmini katika mkondo wa mashtaka, kuangalia jinsi inatofautiana na kesi za kawaida, ni muhimu kuambatanisha mkondo wa mashtaka na mpangilio wa uhamasishaji. Hata kama utapoteza kesi yako, manufaa yaliopo katika uhamasisho wa umma na kuleta msukumo wa mabadiliko kisiasa utakuwa muhimu sana. Kozi hii inaangazia jinsi ya kuunda mpangilio wa uhamasisho kuambatanishwa na mkondo wa mashtaka, kwa kuangazia sheria za kupigana na uzimaji mtandao.
Ni nini nafaa kujua:
Utafaidi sana kutokana na kozi hii iwapo utakuwa na uelewa wa lengo kuu kuhusiana na uhuru wa kuzungumza. Sharti ujue kuhusu ulinzi wa kikatiba wa haki hii, ni mikataba ipi ya kimataifa imeidhinishwa na iwapo kuna sheria ya kimataifa ya fidia kwako. Pia ni vizuri ujue kama serikali yako imejihusisha na uzimaji mtandao, kitaifa au baadhi ya maeneo ya taifa na ni vipi washikadau tofauti wameshughulikia suala hili.

Walimu

Toby Mendel

Toby Mendel is the founder and Executive Director of the Centre for Law and Democracy (CLD), based in Halifax, Canada. CLD works to promote, protect and develop those human rights which serve as the foundation for or underpin democracy, including the rights to freedom of expression, to vote and participate in governance, to access information and to freedom of assembly and association.

1.1 Utangulizi wa kozi
1.2 Utangulizi katika uzimaji Mtandao
2.1 Muhtasari wa kanuni muhimu za uhuru wa kuzungumza
2.2 Vikwazo katika uhuru wa kuzungumza
2.3 Haki ya kusaka na kupokea habari
2.4 Kanuni kuu za uhuru wa kuzungumza
2.5 Swali
3.1 Vigezo vikuu vya mkondo wa mashtaka dhidi kesi za kawaida
3.2 Masuala muhimu ya kuzingatia kabla ya kujihusisha na mkondo wa mashtaka
3.3 Kutumia mkondo wa mashtaka ili kuunga mkono uhuru wa kuzungumza
3.4 Hatua muhimu za kuweka mkondo wa kisheria
4.1 Manufaa na changamoto kuu za kuweka kesi ya uzimaji
4.2 Ni vipi tutaunda mbinu imara ya kesi
4.3 Hoja kuu za kisheria
4.4 Ufafanuzi zaidi kuhusu hoja za kisheria
4.5 Orodha ya mbinu ya kisheria
4.6 Swali
5.1 Umuhimu wa uhamasishaji kwa muktadha huu
5.2 Mfumo wa kuandaa mkakati wa uhamasishaji
5.3 Kisa cha utafiti - MISA Zimbabwe - Helen Sithole
5.4 Vifaa muhimu vya uhamasishaji na malengo ya mkondo wa mashtaka
5.5 Kushirikisha vyombo vya habari
6.1 Vipengele vya kawaida vya muktadha wa kuzima kwa Mtandao
6.2 Changamoto maalum kwa mashtaki ya uzimaji
6.3 Vigezo vikuu katika muktadha wa Uzimaji Mtandao – Na Natalia Krapiva
6.4 Videkezo jinsi ya kushughulikia changamoto
6.5 Swali
7.1 Hitimisho
7.2 Uchunguzi wa kozi

Kozi zinazohusiana

  • 60 dakika

    Shutdown Academy

    Kichwa cha Kosi : Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao

    WITNESS

    60 dakika

    WITNESS
  • Open Observatory of Network Interference (OONI)

    90 dakika

    Open Observatory of Network Interference (OONI)

usomaji unaopendekezwa

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
  • Faragha
  • Maagizo