Jinsi The Economist inatumia IODA kuripoti Uzimaji Mtandao

Mashirika mengi yanategemea data za IODA kwa kuripoti uzimaji mtandao ikijumuisha makundi yanayotekeleza upimaji unaohusiana na udhibiti, mashirika ya wanaharakati, makundi ya uhamasishaji pamoja na mashirika ya haki za binadamu. Vilevile, wanahabari kutoka mashirika mbalimbali ya habari kama vile The Economist, The Wall Street Journal, The Washington Post, Newsy, na Wired  yanatumia data za IODA kufuatilizia na kuripoti uvurugaji wa uunganishwaji mtandao kote ulimwenguni.

Rebecca Jackson, mwanahabari wa takwimu katika gazeti la The Economist, anatumia data za IODA kufuatilizia ukatizwaji wa mtandao katika vita vya Ukraine. Aligundua uwepo wa IODA kwa mara ya kwanza wakati kuanza kwa vita vya Ukraine.

Nilipendezwa na kufuatilizia ukatizwaji mtandao uliwekwa na Russia na Ukraine, IODA ilikuwa na data muhimu,” alisema.

Jackson aliandika  makala ya takwimu, yaliyoangazia athari pana za uvurugaji mtandao kuhusiana na nchini Ukraine. Alitumia IODA data kuangalia ni miji gani ilikuwa na ukatizwaji mtandao na kwa muda upi.

Kwenye makala haya, mwanahabari anaelezea wasomaji jinsi IODA inafuatilizia uvurugaji huu kwa kuambatanisha taarifa kutoka vianzo vya upimaji. Jackson vilevile alihiari kufikia wanakundi wa IODA kwa ushirikiano zaidi.

Timu ya watafiti wa IODA kwa kweli walikuwa wepesi wa kufanya kazi nao na wa kuwajibika na walinipa data kwa namna ambayo ningefanya kazi nazo,” anasema.

Kufuatia ushirikiano wa mwanzoni na IODA, wakati Jackson alikuwa anaangalia stori – nyingine ya uzimaji kwa wakati huu nchini Syria – aliweza kubaini kuwa serikali ya Syria ilikuwa inafunga mtandao wakati wa asubuhi na mapema kwa saa tatu ili kuzuia wanafunzi kudanganya katika mitihani ya yao ya shule za upili.  

Hii athari kubwa katika uchumi. Na tunashukuru uwepo wa data za IODA, niliweza kufuatilizia halisia wakati ukatizaji unatokea na katika eneo lipi la nchi,”

Hiki ni kisa cha utafiti katika kozi yetu ya ‘Kukagua Uzimaji Mtandao kwa kutumia IODA’, katika kituo chetu cha Internet Shutdown Academy, ambacho kina kozi 10 katika lugha saba, na kufundishwa na walimu kutoka mashirika makubwa. Imeundwa ili kufunza wanaharakati, wanahabari, na yeyote ameathiriwa na uvurugaji na udhibiti wa mtandao.

Kozi zinazohusiana

 • 60 dakika

  Shutdown Academy

  Kichwa cha Kosi : Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao

  WITNESS

  60 dakika

  WITNESS
 • Open Observatory of Network Interference (OONI)

  90 dakika

  Open Observatory of Network Interference (OONI)

Blogu

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
 • Faragha
 • Maagizo