Shutdown Academy

60 dakika

Kutambua Uzimaji Mtandao na IODA

Internet Intelligence Lab
Muhtasari:
Lengo la kozi hii ni kukufundisha kutumia IODA. IODA inatumika kama jukwaa la kutambua muunganisho wa mtandao. Tunasaidia uhuru wa mtandao katika jamii na watumiaji wa mtandao ulimwenguni ili kuthibitisha uvurugaji wa mtandao na ili kuelewa kina cha uvurugaji huo katika eneo na muda. Ili kufaulu tunatoa dashibodi kwa umma wa kuangalia mtandao muda wa 24/7 na kutoa vipimo vya muunganisho wa mtandao katika nchi, eneo na watoaji mtandao.
Kuhusu kozi hii:
Kwanza, tutazungumzia jinsi IODA ilianza, nani anatumia IODA, na kwa nini. Baadaye tutaangalia ni vipi IODA inapima muunganisho wa mtandao. Tutapitia jinsi gani uzimaji mtandao unatokea. Hatimaye, tutakufunza kuhusu dashibodi wa IODA, ni vipi utautumia, na ujifahamishe kutokana na watumiaji wa IODA.
Najifunza nini:
Utajifunza jinsi gani IODA inapima uzimaji mtandao na ni vipi unatumia dashibodi wa IODA kuangalia uzimaji au kuangalia uzimaji wa kihistoria.
Ni nini nafaa kujua:
Kufahamu kuhusu mtandao: Mtandao umeundwa na angavu kadhaa unganishi ambazo hutoa huduma kwa maeneo mbalimbali. Angafu zina miundomsingi yakuonekana ambayo uunganishwa kwayo na uunganisha njia za mtandao kote ulimwenguni.

Walimu

Alberto Dainotti

Alberto Dainotti ni Profesa katika Masomo ya Sayansi ya Kompyuta katika Taasisi ya Masuala ya Kompyuta katika chuo cha Georgia Tech. Utafiti wake ni kuhusiana na uwiano wa upimaji mtandao, sayansi ya data na usalama wa mtandaoni. Dr. Dainotti alianzisha mradi wa IODA mwaka 2011 kupeleleza uzimaji mtandao nchini Egypt na Libya wakati wa Maandamano nchi za Africa Kaskazini.

Amanda Meng

Amanda Meng, aliye na Shahada ya Ushamifu, na msomi wa masuala ya uanaharakati wa data, mchunguzi kuhusu ni vipi wapigania haki za kijamii na mashirika ya mashinani yanatumia data ili kufaulisha mabadiliko kwenye jamii. Amekuwa akifanya kazi katika mradi wa IODA tangu Januari 2022.

1.1 Utangulizi wa kozi
1.2 Kwanini IODA ni muhimu katika jumuiya ya uhuru wa mtandao?
2.1 Kile IODA inafanya na nini haipimi?
2.2 Utangulizi katika upimaji wa IODA
2.3 Swali
3.1 Ni vipi Mtandao huzimwa
3.2 Suala la kupigiwa mfano: Ni vipi The Economist linatumia IODA
3.3 Tukio la kutafitia: Ni vipi IODA inapima uzimaji mtandao nchini Iran
4.1 Ni vipi unatumia dashibodi ya IODA
4.2 IODA katika utekelezaji: vita vya Russia-Ukraine
4.3 IODA katika huduma: Maasi ya Iran September - October 2022
5.1 Vidio ya kumalizia
5.2 Uchunguzi wa kozi

Kozi zinazohusiana

 • 60 dakika

  Shutdown Academy

  Kichwa cha Kosi : Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao

  WITNESS

  60 dakika

 • Open Observatory of Network Interference (OONI)

  90 dakika

  Open Observatory of Network Interference (OONI)

usomaji unaopendekezwa

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
 • Faragha
 • Maagizo