Shutdown Academy

60 dakika

Utangulizi kuhusu uzimaji mtandao

Access Now
Muhtasari:
Kozi hii inakupa utangulizi kuhusiana na kuzimwa kwa mtandao, ikiwa pamoja na kuangalia tatizo la uzimwaji na mifano ya namna mbalimbali serikali zinazima mtandao na njia nyinginezo za mawasiliano. Itachunguza jinsi uzimaji mtandao unazidisha dhuluma dhidi ya haki za binaadamu na kuzuia mchakato mzima wa kidemokrasia. Kozi hii inaangazia ni nani anapinga, na mbinu kadhaa za washikadau za uanaharakati zinazotumiwa na muungano wa #KeepItOn ulimwenguni ili kusitisha uzimaji mtandao.
Kuhusu kozi hii:
Hii kozi inalenga kuwafaa mawakili, wanaharakati, wapigakamsa, wanasheria, watetezi wa haki za kibinaadamu, watu binafsi, na wanahabari, kwa uelewa wa jumla ni nini uzimaji mtandao, ni wapi hufanyika, na kwa misingi gani.
Najifunza nini:
Kozi hii tangulizi inanuia kuwapa watetezi wa haki za binaadamu, wanahabari, wanaharakati, na watu binafsi kwa mtazamo wa kujuza ni nini uzimaji wa mtandao, kwa nini na lini unafanyika, na ni mashirika yapi yanashughulikia suala hilo la uzimaji mtandao. Pia itaangazia changamoto za kujaribu kupunguza uzimaji mtandao na udhibiti pamoja na ni vipi uvurugaji wa mtandao unaweza kuathiri demokrasia.
Ni nini nafaa kujua:
Kozi hii ni muhimu kwa yeyote aliye na hamu ya kutaka kuelewa sababu msingi za uzimaji mtandao, kwanini na ni vipi hutokea, na ni vipi kumenyana nao. Access Now ni shirika la kimataifa la haki za kibinaadamu ambalo limejitolea kutetea na kueneza haki za kidijitali kwa watuamiaji waliohatarini kote ulimwenguni. Kwa kuhusisha msaada wa kiufundi wa moja kwa moja, uhusishwaji kamilifu wa kisera, utetezi wa kote ulimwenguni, ufadhili wa mashinani, utumiaji sheria, na makongamano kama RightsCon, tunapigania haki za kibinaadamu wakati huu wa kidijitali.

Walimu

Felicia Anthonio

Felicia Anthonio ni Meneja wa Mradi wa #KeepItOn katika Access Now, shirika la kimataifa lisilo la kibiashara kwa wito wa kueneza na kutetea haki za mtandaoni za watumiaji waliohatarini. Mradi wa a #KeepItOn, ni mradi wa kote ulimwenguni ambao umeunganisha zaidi ya mashirika 280 ambayo yanayojituma kumaliza uzimaji mtandao kote ulimwenguni.

1.1 Utangulizi wa kozi
1.2 Uhalisia wa uzimaji wa mtandao
1.3 Namna uzimaji wa mtandao huvuruga haki za watu
1.4 Swali – Vigezo muhimu vya uzimaji mtandao
1.5 Historia ya uzimaji mtandao – Kutoka Egypt hadi Myanmar
2.1 Kufafanua uzimaji mtandao(ufafanuzi wa #KeepItOn) (Vidio)
2.2 Kiufundi inamaanisha kuzima mtandao
2.3 Swali – Je, ninashuhudia uzimaji mtandao?
3.1 Kwa nini uzimaji mtandao ni kizuizi cha uchaguzi
3.2 Machafuko ya kiraia, maandamano na uzimaji
3.3 Wanaharakati wanapaswa kujua nini
3.4 Tukio La Kupigiwa Mfano - Susan Mwape, Tukio la Kupigiwa Mfano la Common Cause Zambia
3.5 Swali - Zoezi
3.6 Kisa kilichotafitiwa Cuba - Norges Rodríguez, Yucabay
4.1 Vidokezo vya kujiandaa dhidi ya uzimaji mtandao wakati wa uchaguzi na machafuko ya ki
4.2 Kuhusu muungano wa #KeepItOn
4.3 Vifaa angalizi dhidi ya uzimaji mtandao
4.4 Kushirikiana na taasisi za kitaifa na kimataifa dhidi ya uzimaji
4.5 Kwa nini sekta binafsi ni muhimu
5.1 Vidio ya kumalizia
5.2 Uchunguzi wa kozi

Kozi zinazohusiana

  • 60 dakika

    Shutdown Academy

    Kichwa cha Kosi : Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao

    WITNESS

    60 dakika

    WITNESS
  • Open Observatory of Network Interference (OONI)

    90 dakika

    Open Observatory of Network Interference (OONI)

usomaji unaopendekezwa

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
  • Faragha
  • Maagizo