Shutdown Academy

60 dakika

Utetezi na Kampeni Dhidi ya Kuzimwa kwa Mtandao

Access Now
Muhtasari:
Kozi hii inaangazia kuzima kwa mtandao na jinsi ya kuhamasisha na kupigana dhidi ya jambo hilo. Ikilenga mashirika ya kiraia na wanaharakati wa ngazi ya chini, kozi hii inatoa ushauri wa vitendo, mbinu na mikakati ambayo watu binafsi au mashirika yenye rasilimali chache yanaweza kuyatekeleza.
Kuhusu kozi hii:
Kuzimwa kwa mtandao kunaweza kutuathiri sisi kama watu binafsi au wanaharakati katika karibu nyanja zote za maisha yetu, ikijumuisha jinsi wanafunzi wanaweza kushiriki katika mitihani, jinsi waandishi wa habari wanavyoripoti matukio, jinsi tunavyoshiriki katika uchaguzi, jinsi biashara ndogo ndogo zinavyoweza kuhimili na kuendelea na jinsi tunavyopata huduma ya afya. Haya sasa, tuanze safari ya kupanua na kutetea haki za kidijitali za kila mtu.
Najifunza nini:
Kozi hii inakusudiwa kuwapa watu binafsi na vikundi vidokezo vya vitendo vya kampeni za utetezi wa umma dhidi ya kuzima kwa mtandao. Katika kila sura, kozi inaangazia jinsi majimbo, watawala, wanajeshi, na watendaji wengine ulimwenguni kote huwezesha na kutekeleza kuzima kwa mtandao, ikiangazia mafunzo kutoka kwa wale wanaopigana dhidi yake.
Ni nini nafaa kujua:
Kozi hii haihitaji ujuzi wowote maalum. Kwa kuwa inaangazia kuzima kwa mtandao na kuainisha njia za kusuluhisha kuzima, maarifa fulani ya mitandao ya kijamii, mitandao ya simu na majukwaa ya intaneti ni muhimu, ilhali maarifa ya msingi ya IT itasaidia lakini si muhimu.

Walimu

Felicia Anthonio

Felicia Anthonio ni Meneja wa Mradi wa #KeepItOn katika Access Now, shirika la kimataifa lisilo la kibiashara kwa wito wa kueneza na kutetea haki za mtandaoni za watumiaji waliohatarini. Mradi wa a #KeepItOn, ni mradi wa kote ulimwenguni ambao umeunganisha zaidi ya mashirika 280 ambayo yanayojituma kumaliza uzimaji mtandao kote ulimwenguni.

1.1 Utangulizi wa kozi
1.2 Athari za kuzima mtandao
1.3 Kupambana na kufungwa mtandao - mikakati na mbinu za wanakampeni
1.4 Kupambana dhidi ya kufungwa mtandao - mafunzo kutoka kwa kampeni ya #KeepItOn
2.1 Kuzorota kwa demokrasia duniani na kupungua kwa nafasi kwa jumuiya za kiraia
2.2 Kuzimwa mtandao barani Afrika: ni nani anayeziendeleza? Nani anapigana nazo?
2.3 Kuzimwa mtandao huko Asia Pacific: ni nani anayezifanya? Nani anapigana?
2.4 Kuzimwa Mtandao huko Mashariki ya Kati na Afrika Kaskazini: Ni nani anayezifanya?
2.5 Kuzimwa huko Amerika Kusini na Karibiani: Ni nani anayeziendesha? Nani anapigana?
2.6 Kuzimwa mtandao huko Ulaya Mashariki na Asia ya Kati:ni nani anayezifanya?
3.1 Zana za utetezi wa kuangalia uchaguzi na kuzima mtandao
3.2 Kuzimwa mtandao wakati wa machafuko ya wenyewe kwa wenyewe na maandamano
3.3 Kuzima Mtandao wakati wa mitihani
3.4 Kukaa salama wakati wa kuzimwa mtandao
3.5 Shughuli: Je, unaweza kumkabili mhusika wa kusimamisha uchaguzi?
3.6 Kupambana na kufungwa mtandao kupitia taasisi za kimataifa, jumuiya ya kimataifa
3.7 Jinsi makampuni yanavyoweza kupambana na kuzima mtandao Mwongozo wa Umoja wa Mataifa
4.1 Uchunguzi kifani: kuzimwa mtandao na jinsia
4.2 Uchunguzi kifani: kuzimwa mitandao na misaada ya kibinadamu
4.3 Uchunguzi kifani: kuzimwa na ulemavu
4.4 Uchunguzi kifani: kuzimwa mtandao na huduma za afya
5.1 Malizia video
5.2 Uchunguzi wa kozi

Kozi zinazohusiana

 • 60 dakika

  Shutdown Academy

  Kichwa cha Kosi : Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao

  WITNESS

  60 dakika

  WITNESS
 • Open Observatory of Network Interference (OONI)

  90 dakika

  Open Observatory of Network Interference (OONI)

usomaji unaopendekezwa

Ruka enda kwa upitiaji/urambazaji
0
0
 • Faragha
 • Maagizo