Helo!
Tuna furaha kutangaza uzinduzi wa tovuti yetu mpya ya Kiswahili!
Iwapo unaguswa kuhusiana na haki za kidijitali na uhuru wa mtandao, uko katika eneo zuri!
Advocacy Assembly ni jukwaa wazi wa mafunzo ya mtandaoni ambalo liliasisiwa mnamo 2015. Kukiwa na watumiaji kutoka 175 nchi tofauti ulimwenguni, linatoa nafasi kwa watu kusoma ujuzi mpya kama wanaharakati wa haki za binaadamu, wahamasishaji pamoja na wanahabari. Katika Advocacy Assembly, tunajivunia kwa kutoa kozi zenye ubora wa hali juu ambazo zimeundwa kukuimarisha ujuzi wako. Kozi zetu zimehusisha nyenzo mbalimbali za kusomea, kama vile, vidio, mawasilisho, visa vya utafiti, na mifano ya uhalisia-duniani, ili kulainisha kontenti na za kueleweka. Pia, tunatoa maswali na mitihani mwisho wa kila somo kuona uelewa wako na kuangalia maendeleo yako.
Tumeshirikiana na zaidi ya mashirika 20 ili kuzindua kozi mpya kwa lugha tofauti kila mwaka. Tunatoa kozi kwa mada mbalimbali, ikiwa ni pamoja na uhamasishaji, sheria za haki za binaadamu, haki za kidijitali, data za sayansi, usanifu, usalama wa kidijitali, uanahabari wa udukuzi, matangazo, na uzimaji mtandao.
Utangulizi wa Advocacy Assembly Shutdown Academy
Advocacy Assembly ilianzisha Shutdown Academy mnamo 2022. Shule hii inahusisha kozi kumi zinazofundishwa na wataalam wa kimataifa, ziliundwa kuelimisha wanaharakati, wanahabari, na yeyote aliyevurugikiwa na mtandao. Kozi hizi kiasilia ziliwasilishwa kwa Kingereza na zimetafsiliwa kwa Kifaransa, Kihispania, Kireno, Kiswahili, Kiarabu, na Kiajemi.
Muda wote katika Shutdown Academy, utajifunza ni vipi utapima uzimaji mtandao, ni vipi utazikwepa ukitumia vifaa maarufu na mbinu, ni vipi utaanzisha kampeni ya uhasishaji, ni vipi utahusisha sekta binafsi, na ni wakati gani kutumia utaratibu wa mahakama kupinga uzimaji ambao unakiuka sheria.
Kozi zetu & Washirika wetu:
1. Utangulizi kuhusu uzimaji mtandao (Access Now)
2. Kichwa cha Kosi: Kunakili Ukiukaji wa Haki za Binadamu wakati wa Kuzimwa Mtandao (Witness)
3. Kupima Udhibiti Mtandao kutumia vifaa vya OONI (OONI) – yaja karibuni kwa Kiswahili pia!
4. Kutambua Uzimaji Mtandao na IODA (IODA)
5. Kupunguza Udhibiti Mtandaoni (VESinFiltro)
6. Kupunguza Uzimaji Mtandao (VESinFiltro)
7. Kuandaa Mpangilio Tekelezi Dhidi ya Uzimaji Mtandao (Internews)
8. Kampeni za Uhamasishaji wa Umma Dhidi Uzimaji (Access Now)
9. Utaratibu wa Kisheria Dhidi ya Uzimaji (Access Now)
10. Kushauriana na sekta binafsi ili kusitisha Uzimaji Mtandao (GNI)
Baada ya kumaliza kozi, utapata cheti cha kuonyesha mafanikio yako.
Uko tayari kwenye hatua ya kujifahamisha na uhamasishaji? Hapa mna jinsia ya kujihusisha:
60 dakika
60 dakika
90 dakika
Shutdown Academy
90 dakika
Shutdown Academy
Jinsi The Economist inatumia IODA kuripoti Uzimaji Mtandao
Hiki ni kisa cha utafiti katika kozi yetu ya ‘Kukagua Uzimaji Mtandao kwa kutumia IODA’, katika kituo chetu cha Internet Shutdown Academy, ambacho kina kozi 10 katika lugha saba, na kufundishwa na walimu kutoka mashirika makubwa. Imeundwa ili kufunza wanaharakati, wanahabari, na yeyote ameathiriwa na uvurugaji na udhibiti wa mtandao.
Uzinduzi Imara: Gundua Habari Njema katika Advocacy Assembly!
Tunafurahia kutangaza uzinduzi wa tovuti yetu mpya!